Je, kuna wimbo ulikuwa unaupenda sana lakini kulingana na tukio fulani maisha mwako ukatokea kuuchukua wimbo?

Tupakule

Senior Member
Jun 28, 2018
101
409
Wakuu habari za muda huu, natumai mnaendelea vema na majukumu ya kujenga Taifa.

Kama uzi unavyojieleza hapo juu, kuna wakati inatokea tuu kuna wimbo wowote ule uwe wa dini, qaswida, au nyimbo za kizazi kipya au hata cha zamani unatokea kuupenda sana wimbo huo na pengine wimbo huo unakupa/ulikupa faraja sana kwenye maisha yako ukiusikiliza. Je, imewahi kutokea ukauchukia wimbo huo ghafla tuu pengine kwa sababu ya mambo uliyopitia au nyakati ngumu ulizopitia? Na tayari nyakati hizo zimeshapita?

Niende kwenye jambo langu pengine naweza kuwa sijaeleweka nazungumzia nini kwa sababu sio mtaalamu mzuri katika kutoa maelezo.

Mimi kuna wimbo nilikuwa naupenda sana wa Dini umeimbwa na msanii anaitwa Bella Combo, wimbo huu unaitwa "ASANTE".

Baadhi ya maneno yanavyoanza kwenye wimbo huu ni:

"Kwa yale umetenda na yale umefanya, tumekuja na asante Bwana."

Si lugha za malaika, si lugha za watoto wako tumekuja na asante Bwana.

Mwisho wa kunukuu na hii ni baadhi tu ya maneno katika wimbo huo ingawa yapo maneno mengi tuu.

Basi nije kwenye hadithi ya huo wimbo sasa.

Ilitokea siku moja kijana wangu wa kiume alikuwa anaumwa na nilimuguza kwa muda mrefu kidogo almost miaka miwili hivi. Sasa ikatokea siku moja akazidiwa ghafla, nikampeleka hospitali na bahati mbaya akawa amefariki. Mungu ampumzishe kwa amani. Basi nilikuwa na majirani zangu pamoja na kaka yangu tukarudi nyumbani kwa ajili ya taratibu za msiba. Muda huo ilikuwa yapata saa 5 usiku. Basi kufika nyumbani nikakuta majirani tayari wapo nyumbani kwani tuliwapa taarifa. Basi kufika nyumbani baada ya story mbili tatu na kuweka mambo sawa wife akaniita pembeni akaniambia, "toa radio hapo uani ili angalau itusindikize na nyimbo za maombolezo." Nikamwambia sawa basi nikatoa radio uani then nikachukua pc chap nikacopy nyimbo za gospel kwenye flash then nikaweka kwenye radio zianze kuimba.

Wimbo wa kwanza kuanza kuimba ulikuwa wa BELLA COMBO ambao unaitwa "ASANTE." Kwa kweli wimbo huu ulinipa faraja sana ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo katika maisha yetu hasa kwa nyakati niliyokuwa nayo lakini ni wimbo niliokuwa naupenda sana. Basi mambo ya mazishi yakaisha na maisha yakaendelea kama kawaida. Nikirudi kwenye uzi wangu sasa, kila ninaposikia wimbo huu ukipigwa huwa nazima radio au naweka next uje wimbo mwingine na hasa hukunikumbusha tukio la kipindi hicho cha msiba wa kijana wangu na huwa nakosa amani kabisaaa.

Imefikia hatua mpaka nimeufuta kwenye simu yangu, flash na mpaka pc.

Je, kuna aliyewahi kupitia hali hii katika maisha na mwenzangu wewe ilikuwaje na ulifanye?
 
Sina Hizo pigo Kwa kweli napenda mziki japo sio yote na hata nikiuchukia sio kwasababu ya tukio fulani nakuwa nauchukia pengine msanii miyeyusho simkubali.. Hiko ndo ninachokijua
 
Malaika wa Nyanshiski lkn ikawa sivyo siupendi tena,nikiusikia naogopa
 
SIR GOD ..............WIMBO MOJA UNAO REFLECT MAISHA YA VIJANA WENGI ASEEEEE
 
kila wimbo wa zamani ukipigwa lazima ukumbuke ulikuwa kwenye mood ( tukio Gani) whatever ni zuri au baya lakini kwa wapenda music lazima kila tukio liende na wimbo wake
 
Huwa inatokea sana kama nyimbo ya heaven sent ya keyshia Cole,nilikuwa naupenda sana miaka hiyo ila ikatokea moment mbaya sana kwa sasa sitaki na wala sitamani kuiskia.
 
Wimbo wa chid Benz Dar es Salaam stand up🙌🏻, nilikuwa naupenda ila nilipata ajari ya gari halafu nilikuwa nausikiliza
 
Vile vimwansheshi vimeharibu banger moja ya hatar sana saiv sitak hatakuisikia hio ngoma
 
Back
Top Bottom