Amalrik TZ
JF-Expert Member
- Aug 9, 2020
- 341
- 303
Sasa ni rasmi Zanzibar imepata Makamu wa kwanza wa Rais. Hii imetokea siku ya leo tarehe 7/12/2020 baada ya Maalim Seif wa chama cha ACT Wazalendo kula kiapo.
Hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kushika nyadhifa hiyo kwani mwaka 2010-2015 akiwa mwanachama wa CUF pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais.
Wanzanzibar wenyewe walichagua Serikali ya Muundo wa kitaifa na ilipita kwa kishindo kwenye kura za maoni ambapo zaidi ya asilimia 60 waliunga mkono.
Dhima ya Serikali ya muundo wa kitaifa ni kuwaleta wanzibar pamoja na mfumo huu ulianza kutumika toka mwaka 2010.
Lengo la muundo huu wa kiserikali ni jema lakini kwa Katiba ya sasa CCM inapata faida zaidi na vyama vya upinzani vikiambulia patupu.
Tusisahau kwamba CCM ina idadi kubwa ya wajumbe wa Baraza la Uwakilishi huku mkono wa kushoto ukishika Mahaka na wakulia ukiwa na Dola.
CCM kamwe hawataweza kukubali kupatikana kwa sheria za uchaguzi zenye kuleta uhuru na haki nyakati za uchaguzi hilo tuliweke akili kwani kukubali kwao ndiyo kifo chao chama hicho cha kisiasa. Jambo hili ACT Wazalendo wanalijua kwani lipo wazi kwa wote.
Maalim Seif na wenzake wameona isiwe tabu, wamekataa kufa njaa, wamekubali kula, kunywa pamoja na kucheka na watesi wao.
Binafsi jambo hili hajinistua kabisa moyo wangu. Siku ya leo Maalim Seif akiwa anaapishwa alinukuliwa na vyombo vya habari akisema.
“Moja ya yaliyofanya kukubali maridhiano ni imani yetu kwako Rais Mwinyi, vitendo na ishara zako ambazo zimetushawishi kuwa una nia njema na dhamira safi ya kututoa tulipokwama na kuibadilisha Zanzibar yetu katika nyanja zote”.
Najua wananchi wengi wa kawaida ambao walikuwa bado hawajaelewa michezo ya kisiasa inavyoenenda katika nchi hii hawakutemegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye kinywa cha Maalim Seif huku hata siku 50 hazijapita baada ya uchaguzi mkuuu kufanyika.
Lakini ndugu katika ulimwengu wa siasa mambo ndivyo yanavyoenda. Wazungu wana msemo wao unaosema kwamba “If you can’t defeat them, join them” ukimaanisha ukishidwa kuwashinda ungana nao.
Hilo ndilo jambo wanasiasa wanalifanya baada ya kukosa kile wanachokitaka wanabadilika kama upepo. Naamini kila Mtanzania mwenye akili timamu anapenda taifa lenye umoja lakini kwangu mimi umoja ni vitendo na siyo maneno ambayo wanasiasa wanayahubiri majukwaani wakituona sisi kama mazuzu tuyioelewa mambo.
Hawa wanasiasa wa upinzani wakiwa majukwaani katika harakati zao za kutafuta Madaraka wanatuonyesha mambo mauvo ambayo serikali inayafanya lakini pale wakiwekwa kwenye kumi na nane huisifia serikali na kugeuza nyeusi kuwa nyeupe.
Hilo ni somo ambayo nimejifunza katika siasa za Tanzania hasa kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani
Maswali mengi magumu bado yapo moyoni hasa nikiwaangalia wahanga wa uchaguzi ambao wengi ni wananchi wa kawaida wenye kipato duni.
Wapo wananchi ambao wamepoteza maisha na wengine wakipata vilema vya maisha kutokana na hamasa waliyoipata kwa kina Maalim Seif na kujitoa kwa moyo wote kuunga mkono harakati za chama cha ACT Wazalendo.
Binafsi najiuliza, kama jambo hili lilikuwa linawezekana kuzungumnzika mezani kwanini hawa kina Maalim Seif waliwatumia wananchi kama kete ya kupata kile wanacho kihitaji?
Tukumbuke kwamba hii ni mara ya pili kwa Zanzibar kuwa na Serikali ya umoja wa kitaifa. Swali jingine jepesi lenye majibu magumu ni Je, hawa ACT Wazalendo wanauhakika gani kwamba kushirikiana na CCM kutaleta mabadiliko katika chaguzi zijazo?
Ndugu zangu Watanzania itoshe kusema kwamba Wanasiasa wa vyama vyote wanauchu wa madaraka. Uchu wao wa madaraka hupelekea kututoa kafara sisi wananchi wa hali ya chini hasa wenye elimu duni.
Tuweni makini sana na hawa wanasiasa uchwara. Nashauri tuu tuache kuwa washabikia wa hawa wachumia tumbo. Tuungane kwa pamoja na tupiganie kupata Katiba ambayo itatenganisha majukumu ya Serikali, Bunge pamoja na Mahakama hapo ndipo tunaweza kupata mabadiliko ya kweli katika nchi yetu katika nyanja zote.