Je, kila mtu anaweza kuwa tajiri? Ukweli usiosemwa kuhusu uwiano wa maisha

Davidmmarista

JF-Expert Member
Apr 11, 2024
690
1,077
Habari wakuu wa JamiiForums,

Natumai wote mko salama na mnaendelea vyema na harakati za maisha. Leo nina jambo la kufikirisha kidogo, ambalo nataka kulileta mezani kwa mjadala. Hili ni jambo ambalo wengi wetu tunalitazama kwa jicho moja, lakini tukilitazama kwa jicho la pili, tunaweza kuona undani wake halisi.

Hadithi ya Kijiji cha Utopia(Fiction story but has a message inside)

Zamani za kale, palikuwa na kijiji kimoja kilichoitwa Utopia. Kijiji hiki kilikuwa tofauti sana na vijiji vingine vyote. Hapa, kila mtu alitamani kuwa tajiri mkubwa. Watu wa Utopia walikuwa na ndoto moja tu—kupata utajiri wa kupindukia.

Siku moja, mkulima mmoja aliyeitwa Mzee Majaliwa aliamka asubuhi na kusema:

"Nimechoka kuwa mkulima! Hiki kilimo hakinipeleki popote. Nimeamua kuwa tajiri wa madini!"

Kwa haraka, akauza shamba lake na kwenda kuanza biashara ya kuuza madini. Watu wa kijiji walimshangaa, lakini haikupita muda wakaanza kumfuata. Mchinjaji wa kijiji, fundi seremala, na hata mama ntilie waliamua kuachana na kazi zao na kutafuta njia ya kuwa matajiri wakubwa.

Mwaka mmoja ulipita…

Maisha yalibadilika Utopia. Hakukuwa na mtu wa kulima chakula, hakuna aliyebaki kuchinja mifugo, hakuna aliyebaki kupika chakula, na hata fundi wa kutengeneza nyumba hakuwepo. Kila mtu alikuwa anahangaika kutafuta utajiri wake binafsi.

Ghafla, kijiji kilianza kudorora. Chakula kilianza kuadimika, watu wakaanza kufa njaa, na hata pesa walizotafuta kwa bidii hazikuwa na maana tena—kwa sababu hakuna aliyekuwa tayari kuuza chakula, hakuna aliyeosha magari, hakuna aliyepika chakula cha mgahawani, na hakuna aliyefua nguo.

Hatimaye, wakaelewa kitu kimoja…

Katika maisha, haiwezekani kila mtu awe tajiri. Jamii inahitaji uwiano. Lazima kuwe na wakulima, mafundi, wachuuzi, wafanyabiashara, walimu, madaktari, na hata vibarua. Ndiyo maana maisha yamepangwa kwa namna hii—kila mmoja ana nafasi yake.

Ikiwa kila mtu angekuwa tajiri, nani angefanya kazi nyingine muhimu za kila siku? Nani angeuza madafu? Nani angeosha magari? Nani angefua nguo?

Ndio maana kuna maskini, watu wa kati, matajiri, na super wealthy. Mfumo huu unahakikisha kwamba maisha yanaendelea kusonga mbele.

Nimalize kwa kusema,
Mafanikio hayaji kwa kutamani tu kuwa tajiri—yanakuja kwa kuelewa thamani ya kila kazi katika jamii. Siyo kila mtu atakuwa bilionea, lakini kila mtu anaweza kuishi kwa heshima, akifanya kazi yake kwa bidii.

Hivyo, wakuu wa JamiiForums, je, mnakubaliana na falsafa hii? Au kuna jambo ambalo halijaelezwa? Karibuni kwa mjadala!
 
Kuna mtu ambaye ni lazima aajiriwe ili alipwe ujira kwa kuwa hawezi kujisimamia. Mtu wa hivi hata akipata mtaji mkubwa unayeyuka chap chap kama barafu juani. Huyo na utajiri ni kama mbingu na ardhi
 
Nimependa hiyo falsafa ina ukweli ndani yake

Nadhani lazima kuwepo na uwiano huo katika maisha hili kuwepo na madaraja tofauti tofauti katika maisha
 
Serikali duniani kote zinatuhamasisha tujenge uchumi means tuzalishe na ndo maana hata sasa wanawake wa kiislam wanafanya kazi to faut na dini zinavotaka
 
Utajiri sio kitu ambacho kinaweza kuja kwa kupanga japokuwa mara chache hutokea. I second you sio kila mtu anaweza kuwa tajiri na ukiweka sana dhamira ya kuwa tajiri muda mwingine itabidi ufanye hata vitu vibaya ili utimize adhima yako.

Hii ni kusema muda mwingine utajiri unakuja na gharama ambayo unatakiwa uilipe na ukishindwa kulipa gharama ni mateso na majuto tu ndo vitakavyofuatia.

Fanya kazi kwa bidii maarifa na weledi halafu uache utajiri uje wenyewe if you were those few chosen to be a rich man or woman.

"A man called gonamwitu"
 
Back
Top Bottom