Je inawezekana kuijua ID ya mtu kwa kutumia screenshoot aliyoituma au link alizo share mtandaoni?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
4,553
11,570
Habari wakuu,

Kwa mfano tupo kati kati ya mjadala fulani wa michezo nikaamua kuingia google nikaenda kwenye website ya mwanasport ni mfano tu lakini nikascreenshoot picha kama hii hapo chini

Kisha nikaipost humu ili kunogesha mjadala

Screenshot_20240807-185351.png



Inaonyesha muda nilio screenshoot ni saa 12 na dakika hamsini na tatu leo tarehe 16/8/2024

Kikawaida mtumiaji yeyote wa smartphone huwa anatumia gmail yenye majina yake, wengine huweka picha zao kabisa.

Sasa je? Administrator wa mwanasport akijua muda na tarehe niliyoangalia hiyo taarifa
Kisha akaingia kwenye list ya views (wasomaji) akalinganisha huo muda nilioscreenshoot hiyo picha je anaweza kuona email yangu au majina yangu hata kama mimi sio mwanachama wa mwanasport?

Je mtu mwingine asiyehusika akidukua list of viewers anaweza kuona majina ya watazamaji na muda husika tarehe mwezi na mwaka wa viewers wote?

Huu ni mfano tu lengo sio kuchafua taswira ya kampuni yeyote ila ni kutaka kujua kama uwezekano upo! Ili watu humu wawe makini na mambo wanayo screenshoot

Maana nilikaa nikatafakari nikawa sina uhakika

Wataalamu wa IT je hii inawezekana?
 
Na hasa hili suala la kuwa tayari email account iko live, ngoja tujifunze hapa...si ajabu duka la mzungu li wazi..sisi tukidhani tumejisitiri.
 
Back
Top Bottom