Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,626
- 4,273
Mimi siyo mhubiri, ni mtafiti. Lakini naijua kanuni, na kanuni hiyo rafiki yangu, ni Neno la Mungu.
Bwana MUNGU aiambia mifupa hivi; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. (1)
"Mwenyezi Mungu Amtakaye kumwongoza hukifungua kifua chake kwa kunyenyekea. Na amtakaye kumpoteza hukifanya kifua chake kuwa kigumu, kama anayepanda mawinguni. Hivyo basi Mwenyezi Mungu huwalaani wasioamini." (2)
Unajua, watu hawapaswi kuteseka isipokuwa wana hatia. Kiwango cha mateso kitategemea zaidi idadi ya makosa kuliko ukubwa wa kosa moja. Ujinga ni kosa kubwa na upumbavu ndio dhambi kabisa. Dhambi ni UASI. Kuvunja sheria ya kimwili ni kuvunja sheria ya Mungu, vyote ni sawasawa!
E.G. White aliandika barua 30/08/1896:
"Kila matumizi mabaya ya sehemu yoyote ya kiumbe chetu ni ukiukaji wa sheria ambayo Mungu anaipanga itatawala katika mambo haya, kwa kukiuka sheria hii, wanadamu wanajiharibu wenyewe, magonjwa ya kila aina, kuharibikiwa, uozo wa mapema, vifo vya ghafla—haya ni matokeo ya ukiukaji wa sheria za asili."
Hivyo tunakubali: mtu hahitaji kuwa muumini wa mungu-fulani-aliyefumbwa kujua kwamba kuna sheria zinazohusu uhai kwenye ulimwengu huu. Iite Sheria ya Mungu, Sheria ya Asili, Kanuni za Ulimwengu au Mantiki haijalishi. Mkana Mungu na muumini wote huitii.
Ipo sheria ya kupumua kwa viumbe vyote vinavyojongea duniani: vinapaswa kupumua kwa undani na kikamilifu. Kwa takribani dakika tatu mwanadamu hufa akiikana sheria hii. Tukifanya makosa ya kutopumua vizuri kila mara tutateseka kidogo kidogo.
Pamoja na maboresho yaliyopendekezwa katika mifumo ya kidijitali, elimu, miundombinu, nishati, siasa, fedha nk. twahitaji pia kupumua: vizuri na kwa kina wakati wote. Ndiyo Tanzania tunayoihitaji tena sio baada ya miaka 5 wala 25, tunaitaka sasa hivi. Yafuatayo yanaelezea sababu za kuweka kupumua kama kanuni tunayohitaji kutumia kujifungulia uwezo kamili wa kujenga taifa lenye haki, afya na ustawi;
Kiukweli, mtu hawezi kufurahia maendeleo ya taifa bila kwanza kuwa na uwezo wa kupumua. Hapo hatubishani maana tunakubali mtu aliyekufa hana lolote maishani tena. Sasa sizungumzii kutopumua kabisa, nazungumzia kutopumua vizuri.
Mtu hataishi maisha mazuri bila afya. Taifa halitafanikiwa magonjwa yakiliandama. Tuliona jinsi Uviko-19 ilivyosababisha mdororo wa uchumi. Kufanikiwa kuzuia maambukizi ya magonjwa yote bado haitatatosha, taifa linahitaji zaidi ya kukosa matatizo. Maana sio tena kwa ajili ya kutokufa: bali ni kustawi kama watu.
Vuta picha ya tajiri anayefurahia maisha ya utele na afya: hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka. Fikiria matajiri hao wanapambana na masuala ya kuongezeka-uzito: je, bado wanafurahia kikamilifu?
Hivi, kipi hupelekea uzito usiowiana?
Ninapendekeza hiki kama kisababishi toshelevu: Kutopumua ipasavyo kwa hivyo mwili hujirekebisha kwa kuongeza michakato na rasilimali ili kuyaweka maisha vizuri. Itatunza mafuta, glykogeni na oksijeni zaidi ikiwa ni katika kukabiliana na hali iliyopo, amkeni! Kibaya zaidi ni pale mwenye uzito kupindukia akibobea katika sanaa ya mambo yake yote kufanyika huku wakipumua kwa kiwango kidoogo!
Kwa wanaofundisha mazoezi ya viungo: Hakikisheni wateja wanapumua vizuri wakati wa mazoezi ili kuepuka kuongezeka uzito. Upungufu wa hewa ya oksijeni husababisha mwili kuhifadhi chumvi, maji, nishati na kuvuruga homiostasisi. Kama vile 'sensor' za oksijeni kwenye gari, mwili hurekebisha viwango vya oksijeni.
Kuhamasisha upumuaji sahihi kunachochea afya kamili kitaifa, pote vijijini na mijini.
Kuhusu miji: Miji yenye uchafuzi wa hewa huwa na viwango vya juu vya unene na magonjwa yasiyoambukiza. Huenda upumuaji mdogo wa hewa chafu ukachangia matatizo ya kiafya kwa wakazi wa mijini. Je, wakazi wa vijijini hupumua kwa kina zaidi? Utafiti unahitajika. Mabadiliko ya mazingira ni muhimu ili kuruhusu upumuaji kamili wa hewa safi.
Nalitamani taifa ambapo wanasiasa si tu wanafahamu umuhimu wa kupumua kwa usahihi bali pia wanajitahidi kuwa na mazoea hayo, iwe ni kwenye matukio ya umma, maofisini mwao, au wakati wa shughuli muhimu za kitaifa.
Ikiwa mtu amefunzwa kujua kupumua vizuri, atajua na kuchukua hatua wakati wowote kupumua kunapokaribia kuathirika. Ni njia ya moja kwa moja ya kusikia vidokezo na maonyo kutoka kwa dhamiri ndani ya mtu.
Tujiulize kwa nini wanasiasa wanawasilishwa (kikatuni) kuwa wakubwa na wanene kupita kiasi ikilinganishwa na wasio wanasiasa? Yeyote mwenye akili timamu haimpasi kula/kufisadi kiasi cha kuhatarisha upumuaji wake mwenyewe. Wote, viongozi na wananchi tupumue vizuri.
Elimu: Wazazi wanapenda kuwa na watoto wenye akili na afya njema. Walimu wanapenda wanafunzi walio na bidii ya kujifunza. Udadisi ndio akili.
Video: RDNE stock project, Pexels.
Ili kujifunza na kuelewa vizuri, lazima upumue ipasavyo. Watu wasiopumua vizuri mara nyingi hawaelewi mambo. Watu wenye hasira hawasikii vizuri kwa sababu ya kupumua vibaya. Katika migogoro, hakikisha pande zote mbili zinapumua kwa kina kwanza.
Upumuaji na mahusiano: Mahusiano yenye maana hutufanya kuwa na afya na furaha zaidi, kama ilivyoonyeshwa na utafiti wa Harvard (3). 'KataaNdoa' ni genge lililopotoka, poleni. Mahusiano mazuri yanategemea kupumua vizuri. Waliotalikiana hushusha pumzi ndeefu mara baada ya talaka kwa sababu hawakuweza kupumua vizuri pamoja.
Kupumua na afya ya uzazi: Nguvu za kiume na kuridhika kwa wanawake hutegemea afya, ambayo inategemea mzunguko mzuri wa damu na oksijeni. Kupumua ipasavyo huongeza utendaji na kuridhika wakati wa ngono. Wanandoa wanapaswa kujifunza kupumua vizuri, kama vile ngono ya ki'tantric'.
Kama taifa, kujifunza kupumua kwa kina ipasavyo ni muhimu, ingawa sio lazima kuwa wote wana'yoga'.
Tunahitaji tu kujua mbinu hii sahili:
i. Lala, kaa au simama kiutuliiivu.
ii. Pumzisha mwili na akili.
iii. Toa pumzi ndefu ya hewa nje ya mapafu yako.
iv. Kisha vuta pumzi kwa undani sana ukihakikisha kuwa ni upumuaji wa kiwambo/tumbo linainuka na kushuka zaidi ya sehemu zingine za mwili.
Video: Los Muertos crew, Pexels.
v. Rudia mara kadhaa na uifanye kuwa mazoea.
Zoezi hilo la kupumua linasaidia; kupumzika, uponyaji maumivu, usingizi mnono na kuishi kwa amani.
Kama mtafiti, ninaonelea kupumua ni kisababishi toshelevu kuleta matokeo chanya, hata ikiwa pekeyake. Mfano, masikini anayepumua vizuri ana maisha mazuri tayari. WaBongo husema 'AMERIDHIKA'. Vivyo hivyo kwa matajiri.
Katika nchi zilizoendelea, watu wenye ustawi kiuchumi huonana na wataalamu wa saikolojia wanapohisi maisha hayajakaa sawa. Ushauri wa kwanza wanaopewa ni kujituliza kisha KUPUMUA.
Video: Vlada Karpovich, Pexels
Toa pumzi ndefu ukitafakari: 'KWA MUNGU', kisha vuta pumzi ndefu ukijisemea: 'KWA MWANADAMU'.
Je, unafikiri, kupumua ni chanzo? kisababishi? au ni uhusianisho tu? Asanteni.
Rejea:
1. Hezekia 37:5, Biblia Takatifu.
2. Korani Tukufu, 6:125.
3. Harvard Second Generation Study hususani Robert Waldinger's 'TED-Talk'
View: https://youtu.be/8KkKuTCFvzI?si=mNtWlWmrwyyXCMyw