Je, hili limewahi kukutokea? Ulijisikiaje?

Benemention

Member
Jun 9, 2022
38
40
Je umeshawahi kutapeliwa?

Kati ya hizi zifuatazo:-
Twambie ni aina ipi ya utapeli ambayo matapeli wengi hupenda kuitumia hapa Tanzanzia!


1) Wanaojifanya kutoa offer za vifurushi vya mitandao ya simu mtandaoni.

2) Wanaojimilikisha maeneo ambayo sio yao kisha kuyauza! (viwanja & mashamba)

3) Wanaojifanya wapo Zanzibar /Pemba kwa kudeal na uuzaji wa vifaa vya electronics kwa bei nafuu mtandaoni (Instagram & Facebook) kama vile simu na tv!

4) Wazee wa "ile pesa nitumie kwenye namba hii".

5) Wanaojifanya customer care wa mitandao ya simu (Tigopesa, mpesa, airtelmoney).

6) Wauza vitu feki kwa kudai kuwa ni Original.

Kwa mtazamo wako, unahisi ni aina gani ya utapeli imezidi kuchukua nafasi kubwa kuliko zote hizo!!?
 
Juzi kati hivi nilikua Dodoma, sasa nikaona kuna kijiwe kinachoma kuku wa kienyeji, nikauliza bei, jamaa akataka kunipa kuku niliyedhani ni kiporo, nikamwambia hapana, nikachagua kuku mwingine, jamaa akanipiga sound, huyu siyo kuku bali ni kanga, ni mtamu kweli kweli

Aisee, nika change nikamwambie aniwekee huyo huyo, baadae akili yangu ikaakaa sawa, ila alikua mtamu siyo haba, ila jamaa aliniingiza mjini ki-boya sana
 
Back
Top Bottom