Je, Hayati Magufuli alikuwa anatekeleza Ilani ya CCM au alitenda kama mgombea binafsi japo kikatiba haipo?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,082
164,408
Kwenye uchaguzi mkuu option huwa ni mbili kuna wanaochagua chama na Ilani yake na kuna wengine wanachagua mtu bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Kuna wakati RC mstaafu wa Mbeya Albert Chalamila aliwahi kusema kwa utendaji wa Magufuli ulivyo inabidi kianzishwe chama kingine kitakachoitwa Magufuli Ruling Party.

Miezi mitatu baada ya kifo cha Magufuli nimeikumbuka hii hoja ya Mtumbuliwa Albert Chalamila.

Ndio nauliza waungwana yule hayati Magufuli alikuwa anatekeleza ilani ya CCM au aliongoza kwa maono binafsi?

Tazama Mahakama na Bunge zilivyobadilika ghafla.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Tatizo katiba. Katiba hii isipobadilika atakuja chizi mwingine atateuwa mkewe, wanaye, ndugu zake, jirani zake na wanakijiji wenzake kutengeneza serikali, halafu ataamuru tucharazwe viboko 3 kila asubuhi.
Nimesikia tarehe 1 July Ufipa wanaanzisha vuguvugu la kudai hiyo new katiba!
 
Mnataka sasa kuanza kumtenga Magu na CCM maskini, kwamba marosoroso yale yote aliyofanya mnataka kumuangushia jumba bovu peke yake? Si mliona raha kuendesha ma V8 sijui V80 aliyowapa, ni sehemu yenu yule.
Bwashee CCM ni chama kikubwa!
 
Alikuwa anatenda kadri KICHAA chake kilivyokuwa kinamtuma. Ndiyo maana mara inamkuta feri kwa wauza samaki, mara anakula hindi la kuchoma pale Dakawa au unamkuta amelalà kwewnye mawe ya Chamwino kama kenge mwe mimba
Haha umenena mtu wa Mungu.
 
Katiba inavitambua vyama kama wadhamini tu wa mgombea, lakini haisemi chochote kuhusu ilani zao. Akishakuwa Rais, hakuna wa kumpangia tena, msubirini akirudi ndio muulizie "mbona hukutenda kama ilani yako", lakini huwezi kumpeleka mahakamani kwa "kutofuata ilani".

La kujifunza ni kwamba, madaraka ya Rais ni makubwa sana, hata hiyo katiba mpya sio dawa, hata nchi zikiwa na katiba nzuri kiasi gani, kiongozi wa nchi bado anabaki na nguvu nyingi sana. Dawa ni wananchi kuelewa kuwa viongozi lazima wapimwe utimamu kwenye kila kitu ikiwema akili.
 
Kwenye uchaguzi mkuu option huwa ni mbili kuna wanaochagua chama na Ilani yake na kuna wengine wanachagua mtu bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Kuna wakati RC mstaafu wa Mbeya Albert Chalamila aliwahi kusema kwa utendaji wa Magufuli ulivyo inabidi kianzishwe chama kingine kitakachoitwa Magufuli Ruling Party

Miezi mitatu baada ya kifo cha Magufuli nimeikumbuka hii hoja ya Mtumbuliwa Albert Chalamila.

Ndio nauliza waungwana yule hayati Magufuli alikuwa anatekeleza ilani ya CCM au aliongoza kwa maono binafsi?

Tazama Mahakama na Bunge zilivyobadilika ghafla.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Magufuli alikuwa mtawala wa kijeshi kupitia CCM! Ndiyo sababu kila wakati alikuwa anazungukwa na General Mabeyo na IGP Siro!
 
Wafuasi wa mwendazake wachache wanaona haya wanakubali matokeo kua walikua misukule .but wengine wanajidai bdo vichwa ngumu ila moyoni nahis wanajisuta
 
Kwenye uchaguzi mkuu option huwa ni mbili kuna wanaochagua chama na Ilani yake na kuna wengine wanachagua mtu bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Kuna wakati RC mstaafu wa Mbeya Albert Chalamila aliwahi kusema kwa utendaji wa Magufuli ulivyo inabidi kianzishwe chama kingine kitakachoitwa Magufuli Ruling Party.

Miezi mitatu baada ya kifo cha Magufuli nimeikumbuka hii hoja ya Mtumbuliwa Albert Chalamila.

Ndio nauliza waungwana yule hayati Magufuli alikuwa anatekeleza ilani ya CCM au aliongoza kwa maono binafsi?

Tazama Mahakama na Bunge zilivyobadilika ghafla.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Àlitenda kama muhuni tu niamini mimi
 
Back
Top Bottom