Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,953
4,413
Mhe. Hussein Bashe naomba ufafanuzi kidogo kama hautojali.

Kwenye hotuba yako ya bajeti umesema kilimo kilizalisha ajira 475,025 mwaka 2023/24.

1. Unaweza kutusaidia ufafanuzi namna hizi ajira zilivyozalishwa na njia uliyotumia kufahamu kwamba kweli idadi hii ilizalishwa?

2. Kama sekta ya kilimo pekee imezalisha ajira 475,025 mwaka 2023/24, kwa nini Waziri Mkuu kwenye hotuba yake ya bajeti anasema serikali na sekta binafsi kwa ujumla zilizalisha ajira 470,257? Alizisahau ajira za sekta ya kilimo?

3. Katika hotuba yako unasema pia serikali ililenga kuzalisha tani 445,000 za sukari mwaka 2023/24 lakini mkazalisha tani 392,724 na hivyo lengo lilitimia kwa asilimia 85%, lakini takwimu hizi zinapingana na zile zilizopo kwenye ukurasa wa 28 wa Hotuba ya Waziri Mkuu ambaye anasema lengo la kuzalisha sukari lilikuwa tani 555,000 lakini zikazalishwa tani 367,487.54, sawa na asilimia 66.2% ya lengo.

Kwanini wewe unasema lengo la kuzalisha sukari lilitimia kwa asilimia 85% wakati Waziri Mkuu anasema ni asilimia 66% tu?

Kwanini makadirio yako ya lengo kumepungua zaidi ya tani 100,000 ukilinganisha na makadirio ya Waziri Mkuu?

Kwa nini kwenye takwimu zako kuna tani nyingi zaidi zilizozalishwa kuliko zile zilizopo kwenye hotuba ya Waziri Mkuu (wewe ina zaidi ya tani 25,000 ziada)?

Mnapata data kwenye vyanzo tofauti?

Imeandikwa na Edu Talk Tz kutoka mtandao wa X
 
Back
Top Bottom