kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 14,084
- 14,618
Mijadala vyuo vikuu imetoweka, vyuo vikuu vyetu sasa ni sehemu ya kuzalisha vibarua na machawa badala ya fikra. Mhitimu akipewa nafasi ya aina yoyote iwe kazi, uongozi hata ubunge yeye kwake ni kibarua kwaajili ya kulea wanawe tu basi. Hivyo kazi yake itakuwa kusifu, kusifu, kusifu na kujishusha kupitiliza ili kulinda kibarua chake hicho kisimponyoke. Hajali kuwatumikia wale anaowaongoza au kuwapatia huduma bali bali wale waliompatia kibarua. Wengi wao Ni vigumu sana kutumia akili zao wenyewe kuwatumikia wananchi bila kupewa ushauri au maagizo kutoka kwa waliompatia kibarua. Ni Makonda tu peke yake ndiye anaonekana kutumia akili zake katika kutoa huduma kwa wananchi wanaomtegemea.
Msomi wa kweli na mzalendo hawezi kumuona Lissu kama mtu anaekosea kusema "no reform no election", badala yake anatakiwa kumkosoa njia (approach) yake anayotaka kutumia kuleta hayo mabadiliko (reform) kwenye katiba na tume ya uchaguzi. Anachokisema Lissu kuhusu Katiba, Tume na chaguzi viko bayana kwa mtu yeyote hata mwenye D mbili tu, Ila Vyama vya upinzani vinakosa kuungwa mkono na wasomi wetu wengi kwasababu ya hofu waliyotengenezewa kwenye miaka ya hivi karibuni tangu Mwl Nyerere alipong'atuka. Je, tuseme wasomi wetu wakuu nchini wanaona Katiba, Tume ya uchaguzi na chaguzi zetu ziko sawa?
Wasomi wetu wanasubiri muujiza ushuke kuja kutunyooshea kabina, Tume na changuzi zetu? Tuna wasomi ambao wanashindwa kudai hata nyongeza za mishahara yao na kuishia kufanya tafiti kama sehemu ya kipato badala ya kutatua matatizo ya jamii, huku wakisikilizia teuzi.
Shida ya Lissu ni kukosa approach nzuri ya kusema na kutenda mambo. Ni mwanaharakati zaidi kuliko mwanasiasa lakini anazo hoja za msingi. Na iko siku Lissu atakuja kuandika kwenye vitu vyenye hadhi kubwa huko siku zijazo na wako watu wanaoandikwa kwenye vitabu vyenye hadhi leo watakujaandikwa kwenye vitabu vya hovyo kabisa kama watu wabaya sana kwa taifa hili.