Je, CCM ifanye nini kurejesha imani ya wananchi kwao? Kwanini sanduku la kura limeonekana siyo sehemu salama kwao?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,038
4,752
Kwa namna uchaguzi ulivyofanyika ni wazi kwamba CCM wametambua wananchi wengi siyo wakiamini kwenye sanduku la kura.

Alianza JPM alipoona wananchi wanacheka naye lakini inapokuja upinzani wanawapa kura akafuta uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kwa kuuvuruga.

Mwaka 2020 alipoingia kwenye kampeni akaoni wananchi wamesimama na Lisu bila kujali alivyokuwa ametekeleza miradi mingi.akaon isiwe tabu akafyeka wapinzani wote akabaki na CCM pekee.

Mwaka huu tumeona tena mambo yakijirudia, hakukuwa na uchaguzi bali kutimizia wajibu. Mchakato ndani ya CCM ulikuwa siyo wa haki na maeneo mengi viongozi waliopita bila kupingwa siyo even machaguo ya wana CCM. Kwa maana nyingine waliopitishwa siyo viongozi wa wana CCM wala wananchi ni viongozi wa wasimamizi.

Hali hii imenifanya nijiulize ni wapi CCM imewakosea wananchi? Je, wanao mkakati wowote wakijirkrbisha? 2025 naamini pia hakutakuwa na uchaguzi kwa sababu kama kijijini tumepaogopa, je diwani na mbunge tutafanyaje?

Nini hatma ya Tanzania kwenye huu mfumo mpya tulioamua kwenda nao?Tutafika salama au tunajenga nyumba ya matope kwenye mvua?
 
Gentleman,
ile ya muhimu na ya maana sana kwa CCM kufanya, ni kuhakikisha wanamalizia hizo 2% kwenye uchaguzi Mkuu wa 2025, dhidi ya hii 98% ya serikali za mitaa mwaka huu 2024, na hiyo itapendeza zaidi 🐒
 
Back
Top Bottom