Jayrutty Investment kujenga uwanja wa Simba Bunju, uwanja ambao utachukua mashabiki 10,000 hadi 12,000

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,114
2,153
“Jambo la kwanza ambalo tunakwenda kutekeleza ni kujenga uwanja wa mpira, uwanja ambao utachukua mashabiki 10,000 hadi 12,000 na tumekubaliana kwamba Simba wana uwanja Bunju na tutakwenda kujenga uwanja Bunju lakini kama watakuja na mapendekezo mengine basi tutayafata.”

Soma Pia: Klabu ya Simba imesaini mkataba wa bilioni 38 na Kampuni ya JAYRUTTY mzabuni wa utengenezaji Jezi

“Tunajua kwamba Simba makao makuu yapo Msimbazi lakini tunakwenda kujenga ofisi za kisasa. Lakini pia kila mwaka tutatoa Tsh. 100 milioni ya kusaidia kukuza soka la vijana. Kila mwaka pia tutachangia Tsh. 100 milioni kuchangilia pre season. Pia tumeahidi kujenga kituo maalumu cha matibabu ya wachezaji. Kila mwaka pia tutashiriki bega bega katika Simba Day, tutachangia Tsh. 100 milioni kila mwaka.”- Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Jayrutty Investment Company Limited, CPA Joseph Rwegasira

 
..
 

Attachments

  • 20250416_202018.jpg
    20250416_202018.jpg
    31.1 KB · Views: 1
Simba Ina safari ndefu kuwa klabu kubwa Afrika, wamepata ufadhili mzuri, Wana mashabiki wengi Ila kujenga uwanja wa kuchukua watu 10000 sio jambo la kujivunia. Kwa ukubwa wa Simba inahitaji uwanja mkubwa zaidi vinginevyo michuano ya kimaraifa itakuwa inahangika Mara Amani Mara Mkapa au viwanja vipya vitakavyojengwa.
 
Uwanja wa mazoezi na kuchezea Ndondo cup..

Mashabiki 12k ni wachache mno..
 
Back
Top Bottom