Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 519
- 2,925
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.
Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.
Maswali ya kujiuliza.
1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?
2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?
3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?
4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?
Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.
Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.
Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.