Kayombo Tips
JF-Expert Member
- Jun 19, 2020
- 461
- 573
Vijana mmeaminiwa na Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania kwa kupewa uwaziri lakini mnachokifanya kwenye wizara zenu ni madudu tu. Hamjaonesha kuwa mko competent kuweza kugombea nafasi ya Urais hapo mbeleni.
Mwigulu Nchemba umeshindwa kubuni vyanzo vipya vya kodi badala yake umeweka tozo kubwa na Wananchi ndiyo wanaoumia.
Nape Nnauye umeshindwa kudhibiti mitandao ya simu inajipandishia tu gharama za vifurushi. Hebu fikiria ndani ya mwaka huu mitandao ya simu imebadilisha vifurushi na kupandisha gharama za vifurushi zaidi ya mara tatu mfululizo.
Mwaka jana tu, tumenunua vifurushi GB 1 kwa TZS 1000 na 1500, lakini tangu tuanze mwaka huu mpaka sasa hivi vifurushi TZS 3000. Hivi kweli umeshindwa kudhibiti mitandao ya simu isiwe inapandisha gharama kiholela pasipo utaratibu maalumu? Watu wengi siku hizi wanafanya biashara kwa kutumia mtandao wa intaneti, sasa mnapopandisha gharama kiholela hamuoni kama mnazidi kuongeza ukali wa maisha kwa Wananchi?
January Makamba umeshindwa kutafuta majibu ya nishati hapa Nchini. Kila siku umeme unakatika na kuwa wa mgao. Sababu mnazotoa ni kuwa maji machache. Hivi kweli sisi tunategemea maji pekee kuzalisha umeme? Hivi sisi si tuna gesi nyingi tu? Hivi sisi si tuna maeneo mengi yenye upepo wa kutosha? Hivi sisi si tuna makaa ya mawe mengi tu? Kama ni ndiyo hizo sababu za visingizio zinatoka wapi?
Mbona kipindi cha Magufuli umeme ulikuwa haukatikati kila siku kama sasa hivi? Kuna hujuma mnafanya nyie. Huwezi kutoka waziri na kutoa sababu ya kwamba umeme ni wa mgao kwa sababu ya upungufu wa maji wakati tuna njia nyingi za kupata umeme.
Linakuja suala la maji. Hivi kweli sisi ni wa kuwa na mgao wa maji wakati tumezungukwa na maji kila kona? Hapa Dar ES Salaam tumezungukwa na bahari, lakini mmeshindwa kutengeneza mifumo bora ya kupata maji?
Mpaka sasa ni dhahiri kwamba CCM imeshindwa kwa kila kitu. Haiwezekani kama CCM ipo, inaruhusu mambo ya hovyo kama haya yaendelee kutokea.
CCM na nyie vijana niliowataja hapo juu tutawahukumu hapo mbeleni kwa uzembe mnaoendelea kuonesha sasa hivi kwenye uongozi wenu.
Mwendo huu mnao enda nao, endeleeni kwenda nao mpaka mwaka 2025. Natoka mimi.