ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,676
- 69,306
Mwaka Jana Serikali ya Tanzania ilisema inaenda kufufua Mradi mkubwa wa kujenga Ukumbi mkubwa wa Mikutano ya Kitaifa Kwa jina la Kilimanjaro International Convention and Exhibition Centre-KICC Arusha ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Washiriki zaidi ya 3,000 Kwa Ajili ya kushindana na Kenya, Rwanda kwenye biashara ya Utalii wa Mikutano.
Sasa alivyoingia bwana Makamba Amefuta Mradi huo na badala yake amekuja na plan ya kuanza kujenga majengo makubwa aliyoita ya kibiashara na ya kupangisha kwenye Nchi zingine Kwa kutumia viwanja vinavyomilikiwa na Balozi zetu.
Mfano anasema Serikali utajenga jengo la Gorofa 22 Nairobi Kenya
Itajengwa jengo la Gorofa 25 Kinshasa
Gorofa 18 Lusaka Zambia nk
Hivi na Nchi zingine zinafanya mambo ya ajabu kama hivi? Yaani badala ya kuendeleza kwenu mnajenga Miji ya watu Kwa maelezo kwamba mtapangisha.
Binafsi siungi mkono Mpango huu naona kama ni ufujaji wa pesa za Umma.Tujenge kwetu Kwa manufaa ya Watanzania.
----
TANZANIA KUVUNA TSH 36B KILA MWEZI UJENZI WA MAGHOROFA NJE YA NCHI
Serikali kwa mwaka wa fedha ujao, umepanga kujenga majengo ya kiuchumi katika majiji ya Kinshasa (DRC- ghorofa 25) na Nairobi (Kenya- ghorofa 22).
Picha za majengo ya Nairobi na Kinshasa zipo tayari na picha za majengo mengine ya kitega uchumi katika majiji ya Maputo (Msumbiji), Bujumbura (Burundi), Kigali (Rwanda) na Lilongwe (Malawi) nayo imewekwa wazi.
Hayo yamesemwa leo Jumanne Mei 28, 2024 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba wakati akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Wizara imeliomba Bunge kuidhinisha Sh241.069 bilioni ambapo kati ya fedha hizo Sh229.4 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh11.6 bilioni ni kwa ajili ya bajeti ya maendeleo.
Maombi hayo ya fedha ni pungufu kwa asilimia tatu ikilinganishwa na bejeti iliyopita na hiyo imetokana na kupungua kwa fedha za maendeleo kwa asilimia 34.
Kwa mujibu wa Makamba, Serikali ina nyumba na viwanja 109 dunaini kote na kodi ya pango wanayolipa ni Sh29 bilioni kwa mwezi.
Amesema uwekezaji huo ukikamilika utaingiza Sh36 bilioni kwa mwezi na kwa mwaka Sh692 bilioni.
View: https://www.instagram.com/reel/C8WpysQtF8v/?igsh=MXJ2bmgzcWh2MHN2Nw==