January alikuwa boss wa DGIS wa sasa, alikuwa bosi wa Waziri mpya wa Mambo ya Ndani. Je, aliwahi kuwakosea heshima?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,020
4,698
Waziri wa Mambo ya Nje ni bosi wa Mabolizi wote Duniani. Bolozi ni vituo vya kazi ambavyo Waziri anavisimamia.

Uteuzi wa DGIS umeenda sambamba na kuondoa mabosi wake wa zamani ofisini yaani Waziri na Naibu waziri huku KM akibaki.

Je, kuna namna January amewahi kuwakosea heshima wazee hawa wazalendo kwa Taifa letu? Kama amewahi kuwakosea, anafahamu kwamba aliwafanyia ubaya?

Wadadisi wa mambo tudadavulieni, siku zote uteuzi unaambatana na kusafisha ofisi.....je ofisi za umma kwa uozo ulipo bado baadhi ya mawaziri watakuwa salama?

Tukumbuke mama amewaweka washauri wake mbali wasigundulike na ndiyo maana hakuna kuvuja kwa taarifa now days. Vigogo hawana tena breaking news.

Natafakari kwa hali ya utekaji inayoendelea na ujio wa mwanadiplomasia huyu kwenye ofisi nyeti....wakuu wa vyombo vya dola na wizara husika wanaweza wakawa salama kwenye pangua pangua?

PIA SOMA

- Kuelekea 2025 - Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Back
Top Bottom