Apr 28, 2017
27
59
Malaria, Typhoid na UTI ni magonjwa ambayo yanaongoza kwa kuwa ‘diagnosed’ kwa maana nyepesi ni magonjwa ambayo utaambiwa unayo mara nyingi kama si mara zote unapokwenda kupima katika hospitali au maabara hasa hizi ndogo ndogo za mtaani.

Magonjwa haya kwa mujibu wa repoti za ‘ndomo’ na takwimu za mamlaka husiku, magonjwa haya yameshamiri sana. Malamka husika ilirepoti kuwa haya magonjwa yamekuwa ‘overdiagnosed’ yaani watu wengi wameambiwa wanayo mpaka inatia mashaka kama ni kweli wanayo haya magonjwa.

Baadhi ya maswali ya muhimu ya kujiuliza ili kupata ukweli wa hili janga ni; je ni kweli unakua na haya magonjwa au unaishia unapachikwa tu? Je maabara hizi zinafanya vipimo stahiki vyenye uwezo wa kugundua haya magonjwa? Je maabara hizi zina wataalam wenye uwezo wa kutafasri majibu ya vipimo hivi kwa usahihi? je kuna quality assurance ya kutosha kuweza kuthibit ubora wa huduma katika maabara hizi?


Sababu au maswali yote hapo juu yanaweza kwa namna moja au nyingine kuathiri majibu ya vipimo na hatimaye majibu ya ugonjwa utakaoambiwa unao
.
Je ni zipi dalili za magonjwa haya zinazoweza kukupa ‘clue’ au mwanga juu ya ugonjwa unaoumwa?

ANGALIZO dalili za magonjwa zinaweza kufanana au kuelekeana na si lazima kila mgonjwa awe na dalili hizi zote.

Tukianza na Malaria, japo ugonjwa huu bado upo ila umepungua sana ikilinganishwa na hapo zamani, dalili za malaria zinaweza kuwa moja kati ya hizi au nyingine ambazo hazijatajwa hapa; homa, kichwa kuuma, kutapika, degedege, viungo kuuma, kupoteza fahamu, n.k.

Kipimo cha awali kitakuwa cha Malaria Rapid diagnostic test ‘MRDT’ kikiwa positive ni muhimu kupima kipimo cha ‘BS’ Blood silde ili kuangalia idadi ya wadudu, kwa maana rahisi ni kuwa mtaalam wa afya hawezi kukwambia idadi ya wadudu kama hana darubini/hadubini.

Mpimaji akipima kipimo kinachofanana na kile ha kupima VVU/ UKIMWI alafu akakwambia idadi ya wadudu wa malaria mfano sijui watatu au wanne jua huo ni uongo, kimbia hiyo sehemu.

Typhoid ni ugonjwa siriazi kidogo,unaweza ukawa na homa, kutapika, kuharisha, tumbo kuuma na nyinginezo nyingi, lakini dalili moja muhimu y augonjwa huu ni homa inayokuwa inaongezeka kadri siku zinavyosogea, kwa jina la kiingereza ‘step ladder fever’ yaani ukilinganisha homa ya leo ni kubwa kuliko ya jana, na kesho itakuwa kubwa kuliko ya leo, kipimo sahihi cha ugonjwa huu ni kuotesha damu maabara, majibu yakuotesha damu maabara ‘blood culture’ yanachukua siku tatu mpaka tano kwa wastani, hivyo mtaalam wa afya akikupima alafu akakupa majibu ya typhoid hapohapo jua kuwa ni uongo na umepigwa.

Mwisho UTI, kitaalam ‘Urinary tract infection’, ugonjwa huu unaweza kuwa na dalili mbalimbali ikiwemo joto la mwili kuwa juu, kutapika, mkojo kuwasha, kuhisi maumivu wakati wa kukojoa, kiuno au tumbo kuuma hasa sehemu ya chini pamoja na nyinginezo, kipimo cha awali kitakuwa kupima mkojo yaani kitaalam ‘urine analysis’, au mkojo kuoteshwa maabara kama itahitajika.

Changamoto kubwa sana ipo kwenye kutafsiri majibu ya kipimo hiki maana sio kila mtaalam wa afya anauwezowa kutasfiri kwa usahihi majibu ya kipimo hiki.

Mwisho wa yote ni muhimu kupata ushauri wakitaalam pale unapokuwa hujisikii vizuri lakini pia ni muhimu kupata huduma katika vituo vyenye reputation ya kutoa huduma bora za afya.
 
Back
Top Bottom