Jana pale Kisutu iliunguruma kesi ya uchochezi namba 11805/2024 Jamhuri dhidi ya Malisa na Boniyai

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,537
7,711
Jana pale Kisutu iliunguruma kesi ya uchochezi namba 11805/2024 Jamhuri dhidi ya Malisa na Boniyai. Jamhuri iliwakilishwa na Mawakili Clemence Kato na Cathbert Mbilinyi. Upande wa utetezi uliwakilishwa na Mawakili Peter Kibatala, Hakima Mwasipu, Dickson Matata, Michael Lugina, Josephat Msanga na Gloria Ulomi. Kwa kifupi upande wa Utetezi ulikua full package.
1743858410433.jpg


Jamhuri ilileta mashahidi wawili, mmoja mhudumu wa mochwari na mwingine askari polisi. Ifuatayo ni sehemu ya cross-examination kati ya shahidi wa Jamhuri na Mawakili wa Utetezi.

KIBATALA: Shahidi unaitwa nani?

SHAHIDI: Mwita Charles Gimoge

KIBATALA: Umri wako?

SHAHIDI: Miaka 31

KIBATALA: Unafanya kazi gani?

SHAHIDI: Mhudumu wa mochwari.

KIBATALA: Kituo chako cha kazi?

SHAHIDI: Hospitali ya rufaa ya Amana.

KIBATALA: Umesomea wapi?

SHAHIDI: MUHAS

KIBATALA: MUHAS ni nini?

SHAHIDI: Muhimbili University of Health and Allied Sciences

KIBATALA: Level gani na course gani?

SHAHIDI: Basic certificate in mortuary attendant

KIBATALA: Ulihitimu Mwaka gani?

SHAHIDI: Mwaka 2021. Lakini pia nilisoma diploma ya clinical medicine japo sikumaliza.

KIBATALA: Kwa hiyo wewe ni Clinical Officer au Mortuary attendant?

SHAHIDI: Mortuary attendant.

KIBATALA: Una uzoefu wa kazi wa miaka mingapi?

SHAHIDI: Miaka minne.

KIBATALA: Tutajuaje kama kweli wewe ni mhudumu wa mochwari katika Hospitali ya Amana?

SHAHIDI: Kwa sababu nafanya kazi hapo.

KIBATALA: Tutajuaje kama kweli unafanya kazi hapo?

SHAHIDI: Ni kweli nimeajiriwa Amana.

KIBATALA: Una kitambulisho cha kazi?

SHAHIDI: Sijatembea nacho.

KIBATALA: Una barua ya utambulisho kutoka kwa mwajiri?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Sasa mahakama hii itaaminije kama kweli wewe ni mtumishi wa Amana?

SHAHIDI: Mkiwapigia simu viongozi wangu watatibitisha.

MAHAKAMA: (kicheko)

KIBATALA: Hapa tunakuuliza wewe, siyo viongozi wako. Kwani unaona viongozi wako hapa?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Sasa Mahakama itaaminije kama wewe si shahidi wa mchongo?

Wakili wa Jamhuri anasimama kuonesha ana hoja kinzani, Kibatala anakaa.

JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu, shahidi ameshajibu kuwa waulizwe viongozi wake. Sioni sababu ya Kibatala kung'ang'ania swali hilo.

KIBATALA: Mheshimiwa, naomba Wakili atulie. Yeye ameshamuongoza Shahidi, sasa ni zamu yangu kumhoji.

HAKIMU: Shahidi, jibu kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Una nyaraka zozote za uthibitisho wa kufanya kazi Amana? Jibu ni rahisi tu, unazo au huna?

SHAHIDI: Sina.

MAHAKAMA: (vicheko)

KIBATALA: Sasa kwanini ulikua unanipotezea muda? Tafadhali eleza mahakama hii utaratibu wa mwili kuingia mochwari pale Amana.

SHAHIDI: Inategemea kama mwili unatoka ndani ya hospitali au nje.

KIBATALA: Elezea kwa mwili uliotoka nje.

SHAHIDI: Mgonjwa au majeruhi akiletwa anaanzia mapokezi, kisha emergency, na baada ya daktari kuthibitisha kifo, mwili unaletwa mochwari kwa ajili ya kuhifadhiwa.

KIBATALA: Je, mwili unapotoka mapokezi unaandikishwa?

SHAHIDI: Ndio. Wanandikishwa wote.

KIBATALA: Nani na nani?

SHAHIDI: Marehemu na ndugu aliyeleta mwili.

KIBATALA: Tuambie tarehe 11 Aprili 2024 ulikuwa wapi na nini kilitokea?

SHAHIDI: Nilikuwa kwenye majukumu yangu Hospitali ya Amana. Akaja Sajenti wa Polisi ambaye nilimtambua kwa jina la Afande Jamada akiwa na mwili.

KIBATALA: Alikuambia mwili huo ni wa nani?

SHAHIDI: Alisema ni wa mtu aliyepata ajali ambaye hakua ametambulika.

KIBATALA: Nini kilitokea?

SHAHIDI: Nikamwambia nafasi zimejaa, kwa hiyo aende Hospitali ya Kilwa Road.

KIBATALA: Kwa nini Kilwa Road na sio Muhimbili au Temeke?

SHAHIDI: Kwa sababu ni moja ya hospitali ambazo huwa tunawaelekeza kwenda kama Amana imejaa.

KIBATALA: Unaijua Kilwa Road ilipo?

SHAHIDI: Hapana, lakini huwa tunaelekeza watu huko kama tumejaza.

KIBATALA: Kwahiyo unaelekeza watu kwenda mahali ambapo hupajui?

SHAHIDI: Hata Temeke na Muhimbili tunawaelekeza pia.

KIBATALA: Rekodi za Amana zinaonyesha kuna mwili uliletwa tarehe 11 April 2024, lakini kwa kuwa mochwari ilikuwa imejaa, mkaupeleka Kilwa Road?

SHAHIDI: Kama mwili haujashushwa, hauingii kwenye rekodi.

KIBATALA: rekodi zipo au hazipo?

SHAHIDI: kama mwili haujashushwa hauingii kwenye rekodi.

KIBATALA: Usijitungie swali. Rekodi zipo au hazipo?

SHAHIDI: Hazipo.

KIBATALA: Umesema maiti iliyoletwa tar 11 April 2024 haikushushwa kwenye gari?

SHAHIDI: Ndio.

KIBATALA: Mlijuaje ni maiti?

SHAHIDI: Kwa sababu niliambiwa marehemu alifariki kwa ajali.

KIBATALA: Shahidi, elewa swali. Aliyekuambia huyo mtu ameshafariki ni nani?

SHAHIDI: Afande Jamada.

KIBATALA: Afande Jamada alijuaje kama huyo mtu amefariki?

SHAHIDI: Alisema alikufa palepale kwenye ajali.

KIBATALA: Ulikuwepo kwenye ajali?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Sasa ulijuaje alikufa pale pale?

SHAHIDI: Afande Jamada alisema.

KIBATALA: Jamada ana utaalamu wa kuthibitisha kifo?

SHAHIDI: Sijui.

KIBATALA: Hujui nani anathibitisha kifo? Huoni hii inaweza kuwa sababu ya wewe kusoma Clinical Medicine ukafeli hukumaliza?

SHAHIDI: Anayethibitisha kifo ni daktari.

KIBATALA: Sasa Afande Jamada alijuaje huyo mtu amekufa wakati hakuna daktari aliyethibitisha?

SHAHIDI: (Kimya)

KIBATALA: Kwa hiyo hamkuingiza mwili kwenye rekodi za hospitali?

SHAHIDI: Mwili haukushushwa kwenye gari.

KIBATALA: Mwili uliingizwa kwenye rekodi za hospitali au haukuingizwa?

SHAHIDI: mwili haukushushwa.

HAKIMU: Shahidi, jibu kama unavyoulizwa.

KIBATALA: Rekodi za huo mwili pale Amana zipo au hazipo?

SHAHIDI: Hazipo.

KIBATALA: Kwa hiyo hakuna ushahidi wa kimaandishi kuwa kuna mwili uliletwa Amana tarehe 11 Aprili 2024? Kweli au si kweli?

SHAHIDI: Kweli.

KIBATALA: Unaweza kuthibitisha ule mwili ulioletwa na Sajenti Jamada ulikuwa mwili kweli au majeruhi ambaye yuko mahututi?

SHAHIDI: Afande Jamada alisema amefariki.

KIBATALA: Mlifanya jitihada za kuthibitisha kitaalamu kuwa amefariki?

SHAHIDI: Hapana.

KIBATALA: Una utaalamu wa kuthibitisha kifo kwa kutazama tu kwa macho bila vipimo?

SHAHIDI: Sina.

KIBATALA: Sasa ulisemaje alikua amefariki?

SHAHIDI: Kwa sababu afande Jamada alisema hivyo.

KIBATALA: Kwanza huo mwili uliuona?

SHAHIDI: niliona kitu kimelazwa kwenye gari.

KIBATALA: Uliona maiti au hukuona?

SHAHIDI: ilikua imelazwa kwenye gari.

HAKIMU: Shahidi nakuonya, jibu swali kama unavyoulizwa.

SHAHIDI: Sikuona maiti Mheshimiwa.

Wakili Kibatala anakaa, anasimama Wakili Hekima Mwasipu.

HEKIMA: Uliona na Sajenti Jamada ana kwa ana?

SHAHIDI: Hapana.

HEKIMA: Sasa ulimwambiaje kwamba nafasi zimejaa?

SHAHIDI: Kupitia dirishani.

Wakili wa Jamhuri anasimama na Wakili Hekima anakaa.

JAMHURI: Mheshimiwa Hakimu, kwa ajili ya kuweka sawa rekodi za mahakama, naomba Shahidi afafanue anaposema hawuonana ana kwa ana anamaanisha nini?

HAKIMU: Shahidi, fafanua.

SHAHIDI: Nilimuona kupitia dirishani.

HEKIMA: unaelewa nini kuhusu ana kwa ana?

SHAHIDI: ni kuonana na mtu moja kwa moja unaweza hata kumshika.

HEKIMA: Sajenti Jamada alileta mwili hadi mochwari akiwa peke yake?

SHAHIDI: Ndio.

HEKIMA: Umesema utaratibu unaanzia mapokezi, sasa yeye aliwezaje kuja hadi mochwari bila kupita mapokezi?

SHAHIDI: Kwa sababu mochwari hakukua na nafasi.

HEKIMA: Alijuaje mochwari hakuna nafasi bila kupita mapokezi?

SHAHIDI: Kama nafasi zimejaa, hakuna haja ya kuandikishwa mapokezi.

HEKIMA: Kwahiyo alikuja moja kwa moja na gari lenye maiti hadi mochwari na kuuliza kama nafasi ipo?

SHAHIDI: Ndio.

HEKIMA: Hospitali ya Amana mtu anaweza kuleta maiti na akaondoka bila kuingia kwenye rekodi?

SHAHIDI: Maiti haikushushwa kwenye gari.

Wakili Hekima anakaa, anasimama Wakili Dickson Matata.

MATATA: Ni miili mingapi iliyokuwepo siku hiyo ya tarehe 11 April 2024?

SHAHIDI: Sikumbuki.

MATATA: Sasa unasemaje mochwari ilikuwa imejaa wakati hujui idadi ya miili iliyokuwepo?

SHAHIDI: Hadi nipitie roster ya siku hiyo.

MATATA: Umekuja nayo?

SHAHIDI: Hapana.

MATATA: Sasa mahakama itaaminije kama kweli mochwari ilijaa bila nyaraka za kuthibitisha?

SHAHIDI: Ni kweli nafasi zilikuwa zimejaa.

MATATA: Mwambie Hakimu apuuze maelezo yako maana hayana ushahidi wowote wa nyaraka.

SHAHIDI: nyaraka zipo.

MATATA: ziko wapi?

SHAHIDI: zipo Amana.

MATATA: Sasa mwambie Hakimu kuwa umekuja na maneno matupu, huna nyaraka za kuthibitisha usemayo.

SHAHID: kimya

MATATA: Shahidi mwambie Hakimu umekuja na maneno bila nyaraka. Kweli au si kweli?

SHAHIDI: Kweli.

MATATA: Ni hayo tu, Mheshimiwa Hakimu.

Shahidi wa kwanza amemaliza. Tukutane jioni kuona Shahidi wa pili akipewa haki yake ya Kikatiba na Mawakili Wasomi.

Courtesy of Brother Malisa 😊
 
watu wanawatetea mpaka kuchanga pesa zao mnapofungwa jela. wengine wana uwawa na kupotea kwasababu ya CHADEMA. Leo mnapingana na mtazamo na msimamo wa waliowengi waNO REFORMS NO ELECTION? AT mnataka kugombea/kuuza majimbo ili mabwana zenu wapite bila kupingwa?
mnatufanya sie wajinga kwa kuwaunga mkono kwa hali na mali kwaajili ya CHADEMA
Watu wamepoteza mpaka kazi kwa ajili ya CHADEMA leo anatokea mjinga mmoja ati G-55 SHENZI
NO REFORMS NO ELECTION
 
Back
Top Bottom