JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 679
- 1,101
JamiiForums imeendesha mafunzo ya siku 2 kwa watumishi na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), yakijikita katika Ushirikishwaji wa Umma, Mbinu za Upigaji Picha, Mawasiliano Salama, na Usalama wa Kidigitali.
Mafunzo haya yalilenga kuwapa washiriki ujuzi muhimu wa kuboresha mikakati yao ya mawasiliano, kuhakikisha usalama wa Kidigitali, na kushirikiana vyema na umma katika zama za Teknolojia.