JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 677
- 1,098
Fuatilia moja kwa moja mjadala unaofanywa na JamiiForums kwa kushirikiana na StarTV kuhusu hali ya siasa Nchini, na utawala wa sheria kuanzia saa 3:30 Usiku mpaka saa 5:30 Usiku.
Washiriki ni;
1: Wakili, Boniface Mwabukusi - Rais wa TLS.
2: Ado Shaibu - Katibu Mkuu ACT WAZALENDO.
3: Benson Kigaila - N/Katibu Mkuu Bara - CHADEMA
4: James Mbatia - Mwanasia Mkongwe, Mbunge wa Zamani, na Mwenyekiti wa zamani wa NCCR MAGEUZI .
5: Michael Urio - Naibu Meya wa Kinondoni, Diwani kata kunduchi - CCM.
Chief Odemba: Malalamiko ambayo wapinzani wamekuwa wakitoa mara kadhaa na hali ya siasa nchini, shida kubwa unadhani ni nini? Je wapinzani wenyewe nyinyi kama nyinyi ndio tatizo kuu au tatizo linatoka Mheshimiwa Benson?
Benson KIgaila: "Wapnzani hatuwezi kuwa tatizo. Tatizo la siasa zetu ni sheria tunajua kwamba kabla ya Magufuli kulikuwa na sheria mbaya za Uchaguzi lakini angalau kulikuwa na nafuu kwa sababu sheria za uchaguzi za wakati ule wote zilikuwa ni sheria na mifumo tuliyoirithi wakati wa chama kimoja.
Sasa tulikofika kimsingi hatuwezi kusema siasa hizi zinarudi nyuma, Siasa za leo zinaingia kaburini na aliyeanza kuziingiza kaburini ni magufuli na Samia anahitimisha. Samia na Magufuli hakuna tofauti.
Tofauti ya Samia na Magufuli ni jinsia zao lakini kama ni utekaji ambao aliuasisi Magufuli unafanyika vilevile. Kama ni wizi wa kura, mifumo ya kuiba uchaguzi inafanyika kuliko kipindi cha Magufuli.
Wapinzani sio shida. Sisi tunachosema hakuna chama kinachotaka kupendelewa, tunataka vyama tucheze mchezo huu katika uwanja sawa. Tuwe na tume tuliyokubaliana, tuandike Katiba Mpya ambayo wananchi wameichagua ili tukienda kwenye uchaguzi wa kushinda ashinde wa kushindwa ashindwe"
Chief Odemba: Itakumbukwa ya kwamba wakati ambapo Rais Samia anaingia madarakani hata chama chako kilimpongeza na mlienda mbali zaidi mkampa tuzo. Sasa baada ya muda mfupi tu tena mnabadilika, wafuasi wenu wanashindwa kuwaelewa ya kwamba pengine nyie mnaona kiongozi ni mzuri pale favour inapofanyika kwenu tu?
Benson Kigaila: Kama kuna mfuasi tunachamchanganya atakuwa maeacha kufikiria. Wakati ule Samia kila mtu alimpongeza kwa kauli zake za kutaka kujenga umoja. Leo tunamlaumu kwa matendo yake.
Mimi kipindi kile nilimshauri ajiepushe na machawa. Akijiepusha na machawa anaweza kufanya mawazo yake anayofikiria lakini leo tunamlaumu kwa matendo wakati ule tulimpongeza kwa kauli.
Kwenye mazungumzo yetu sisi ya kutafuta maridhiano walikubali hoja 11. Katika hoja zetu 11 walikubali hoja 4 tu. Tulipoenda kugusa hoja ya katiba, hoja ya reforms ya mifumo ya Uchaguzi na sheria za Uchaguzi maridhiano yaliishia pale.
Chief Odemba: Boniface Mwabukusi, wewe kama mtaalamu wa sheria unadhani mkanganyiko huu unaotokea baina ya vyama vya upinzani pamoja na chama tawala. Unadhani shida ni nini?
Mwabukusi: Tatizo kubwa linaloathiri siasa zetu ni kwamba tumeingia kwenye siasa za vyama vingi, tukibaki na mfumo wa kisiasa wa chama kimoja. Hivyo vitu haviwezi kwenda pamoja.
Tatizo la pili ni militarization of the democratic process. Mfumo wa kuendesha siasa zetu kivita na hili mi naliona sana kwa jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi linaingilia sana shughuli za kisiasa na hili ndio linaloongeza vilio.
Jambo lingine kubwa ni kukosekana kwa maadili ya kitaifa. Tumekosa maadili kiasi cha kwamba hata vitendo viovu hatukemei kwa lugha stahiki. Watu wanapotea na wanatekwa hatukemei.
Chief Odemba: Ado Shaibu, unadhani nini suluhisho kwa chanamoto zinazokumba vyama vya upinzani Tanzania?
Ado Shaibu: Ni lazima tupiganie mageuzi ya kimfumo. Tusikubali tena kurubuniwa au kupewa hadaa kwa maneno matupu. Utashi wa mtu mmoja hata kama mtu huyo ni Amiri Jeshi Mkuu hautatusaidia kutuvusha kwenda kwenye Uchaguzi 2025.
Tulimshauri Rais Samia ni lazima uruhusu sheria zote zinazobania uhuru wa kisiasa hapa Tanzania ikiwemo sheria ya vyama vya siasa na sheria ya vyombo vya habari.
Lingine pia kama hatu-adress suala la Katiba Mpya tutaendelea kuwa tunajidanganya.
La kwanza ni lazima twende kwenye vuguvugu kubwa la umma na ni lazima tuwasukume watawala na CCM wajue kwamba tumekasirika. Ni lazima nyeusi iwe nyeusi nyeupe iwe nyeupe
Chief Odemba: Mnadhani nyinyi kama wapinzani mkijitathmin mnahisi ni wapi mnapokwama?
Kigaila: Naweza kusema ni kutokuwa na umoja ambayo pia ni mbinu ambayo wanaitumia watawala. Kwa mfano tunaongelea uchaguzi wa serikali za mitaa wa juzi lakini kuna vyama vya siasa vinaweza vikakaa vikasema sisi tumeridhika na huo uchaguzi.
Chief Odemba: Unaongeleaje tetesi za ACT Wazalendo kuitwa CCM B?
Ado Shaibu: Mimi kwa kweli nimeitwa hapa Star TV na nimeeleza muda mrefu, hivi sasa nitajibidiisha katika masuala yanayotuimarisha kuiko yanayotutenganisha kwa hiyo hata hayo masuala no comment tujikite kwenye mambo ambayo yatatusaidia
Nishafafanua hapa kwamba hizo ni propaganda ambazo wapinzani wako wanaweza wakakupa jina hili lakini haya yote yanamnufaisha nani? CCM
Chief Odemba: Unadhani nini kinakwamisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya?
Kigaila: Suala la Katiba Mpya halijafika mahali pa watawala kukubali kwenda huko kwa sababu mbili.
Moja hawana utashi wa kisiasa, wanaogopa kwamba Katiba mpya na kuboresha mifumo ya Uchaguzi ndiyo ondoka yao madarakani. Utashi wa kisiasa haupo.
Cha pili, watanzania hajaionesha serikali ya CCM kwamba wana nguvu ya kubadilisha katiba yao, Tukiunganisha nguvu tukaonesha hiyo nguvu ya pamoja na wakajua hii nguvu ni kubwa wataamua hata kama hawataki.
Chief Odemba: Awali CHADEMA mlisema kuwa pasipo kupatikana kwa Katiba Mpya msingeshiriki Uchaguzi. Nini kimebadilika? Huenda hii ni kutokuwa na msimamo kwamba mnasema hivi alafu baadae mnabadilisha?
Kigaila: Sisi tulienda kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu kubwa mbili.
Moja, kwenda kuthibitisha utashi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambao hauko kwenye maandishi ya kwamba uchaguzi utakuwa huru. Tumeenda na tumethibitisha.