JamiiForums app crashes, nini nakosea?

The Mig

Senior Member
Jan 7, 2017
131
217
Salaam wana bodi.

Kama mada inavyojieleza hapo juu.

Nimekuwa natumia JamiiForums App niliyoipakuwa toka google store.
Lakini kwa muda kama wa wiki mbili hivi kila nikiifungua inaleta habari ya crashes na kunitaka nitume ripoti.

Kwa kweli ilikuwa msaada sana kwangu kwa kuweza kupata habari kwa wakati. Hata ningekuwa safarini palipo na mtandao, nimekuwa si mpweke kwa kusoma JF wakati wowote. Sasa inanilazimu kusubiri mpaka weekend ndo nije fika JF kwa kutumia PC.

Naomba kwa wenye uzoefu nijuzeni wapi nimekosea katika handset yangu?
Maana naona nazidi kukosa utamu, hata ule wa vipepeo weusi naona nao nazidi kuupoteza kwani niliishia episodi ya 6 tu.

Nimejaribu kuiondoa na kuirudisha mara kadhaa bila mafanikio (uninstall/install)

Nawasilisha kwenu wana bodi kwa maelekezo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…