Jamii zinawatengeneza wanaume kuwa viongozi kimfumo, wanawake wanahitaji juhudi na sifa za ziada kuwa viongozi bora

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
46,623
66,814
Katika sehemu nyingi za dunia jamii zimekuwa zinawajenga au kuwatengeza wanaume kuwa viongozi kimfumo kwa kipindi chote cha maisha ya binadamu.

Tukichukulia jamii zetu mtoto za sasa kwa mfano mtoto wa kiume ndiye anachunga mifugo porini na ndiye msimamizi wa mbwa nyumbani, haya ni mambo ya kuongoza kwa sababu yanahitaji kutoa muongozo na ujasiri tofauti na kupika, kufanya usafi au kuosha vyombo.

Mtoto wa kiume anacheza mpira na draft ambayo ni mchezo inayohusisha mipango na mikakati tofauti na rede, kombolela au kibaba-mama.

Mtoto wa kiume anajengwa kutokuwa na hisia kali(emotional), anaambiwa asilie hata pale ambapo anapatwa na machungu, sifa mojawapo ya uongozi ni kutoongozwa na hisia(emotions) zaidi katika kufanya maamuzi.

Ukiyatazama haya mambo na mengine utaona katika mfumo mzima wa maisha ya wanadamu, ukuaji wa mtoto wa kiume unamtengeneza katika mazingira ya kuwa kiongozi autmatically.

Katika jamii ya aina hii inakuwa vigumu sana wanawake kuwa viongozi na zaidi sana kuwa viongozi wazuri kwa sababu wanahitaji kuonyesha uwezo wao wa ziada juu ya wanaume ambao kwa maelfu ya miaka mazingira tayari yamewaanda kuwa viongozi, pia wanahitaji kujifunza sana kutoka kwa viongozi wanaume ili wawe bora.
 
Back
Top Bottom