SoC04 Jamii ifanye nini ili kupambana na Taarifa Potofu?

Tanzania Tuitakayo competition threads

Pendragon24

Member
Aug 8, 2018
67
97
Ulimwengu umepita katika zama tofauti tangu uwepo wake hadi sasa tulipo. Zama hizi za sasa za taarifa ni moja kati ya zama ngumu na muhimu sana kwa jamii kwa sababu bila kuwa na taarifa jamii haiwawezi kushiriki katika shughuli yeyote ya kiuchumi na kisiasa ili kujiletea maendeleo.

1.jpeg
1.jpeg

Wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni wanatakiwa kupata taarifa ili waweze kujua mabadiliko katika mihula,mitahala,ratiba za likizo na matokeo ya mitihani ni muhimu sana kwao.

Wakulima wanatakiwa kupata taarifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ili waweze kutathimini msimu wa kupanda na aina ya mbegu itakayoweza kukabiliana na magonjwa.

Wakati wa korona wananchi walitakiwa kupata taarifa ili kujua mwenendo wa ugonjwa na tahadhari wanazotakiwa kuchukua ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Kipindi cha uchaguzi wananchi wanategemea kupata taarifa za wagombea na taratibu zote za mchakato wa uchaguzi ili waweze kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo.

Hata ushiriki wa majeshi katika vita unategemea ukusanyaji wa taarifa za adui, serikali pia ili kuwahudumia wananchi ni lazima wapate taarifa za mahitaji ya wananchi katika eneo husika,hata katika maisha yetu kila mtu alipo ni muhimu sana kupata taarifa.

Katika zama hizi za taarifa tumeona maboresho makubwa si tu ya kiteknolojia lakini pia ubunifu na ujuzi wa watu waliomo ndani ya vyanzo vya habari kupitia redio, televisheni, magazeti, intaneti na mitandao ya kijamii jinsi ya kutafuta,kuchakata, kuhariri na kuhabarisha umma.

Pamoja na maboresho makubwa ya kihabari lakini bado wananchi wengi kwa sasa wanakabiriwa na wimbi kubwa la ulaji wa taarifa potofu zinazozalishwa na utitili wa vyombo vingi vya habari vilivyopo duniani.
WhatsApp Image 2024-06-07 at 11.30.52.jpeg

Baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiongeza taarifa zao zisizo haririwa katika habari iliyokwisha kuhaririwa na kupelekea taarifa nzima kuwa potofu, zipo baadhi ya redio na televisheni na hata magazeti hayafanyi uchunguzi wa kutosha wa taarifa kutoka chanzo sahihi, mitandao ya kijamii ndio chanzo cha taarifa zao kwa sasa.​

Papa Francis alipotembelea nchi ya DR Congo katika jimbo la Kiivu alisema waziwazi kwamba vyombo vya habari haviandiki ukweli kuhusu hali halisi ya kile kinachoendelea nchini humo.
2.jpeg

Taarifa hizo za uongo na upotoshaji zina madhara makubwa kwa ustawi wa watu maana maisha ya watu ambayo kwa sasa yanategemea taarifa ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika kazi,afya,biashara,usafirishaji,ujenzi,ulinzi na hata katika michezo na njia pekee za wao kupata taarifa za kweli ni redio,televisheni na mitandao ya kijamii.​
3.jpeg

Watu wengi wamejengwa katika kuamini kwamba redio, televisheni na magazetini ndio vyanzo sahihi na vyakuaminika vya taarifa. Wengine wanafikiri kwamba jambo likisemwa na kiongozi, mtu au ukurasa maarufu mtandaoni basi taarifa hiyo ina kweli kumbe ni rotten news.​
4.jpeg
4.jpeg

Serikali nyingi duniani hasa za kiafrika zinafikiri kwamba kuzima intaneti, kufungia vyanzo vya habari, adhabu kali kwa waandishi na kuzuia baadhi ya taarifa kwenda kwa umma ndio njia pekee ya kupambana na taarifa potofu kumbe kwa kufanya hivyo wana haribu na kuzima uhuru wa watu kutoa maoni yao.

Sheria na kanuni ambazo serikali inatunga hazilengi kusaidi jamii dhidi ya upotoshaji badala yake sheria hizo zimekuwa kandamizi kwa waandishi na jamii pia zimetengeneza mianya ya baadhi ya viongozi kuamua ni taarifa gani inapaswa kwenda kwa umma na taarifa ipi haitakiwi kwenda kwa umma.

Matumizi ya fact check ndio njia ambayo watu wengi wanaitumia ili kuhakiki taarifa, lakini tukumbuke kwamba hizi fact checks zinaweza kutawala akili za watu kama ilivyokuwa (redio,televisheni na magazeti) wakiamini kwamba ndio vyanzo sahihi vya kujua taarifa za ukweli kumbe hizi ni software ambazo zinaweza kuingiliwa na virusi zika collapse na kuanza kuzalisha taarifa za uwongo.

Lakini hizi fact check zinaweza kuja kuthibitiwa kisheria kama vyombo vingine mfano redio na televisheni zikawa zinahakiki taarifa za kundi fulani tu la watu. lakini pia fact checks nyingi duniani hazina data za kutosha ili kuweza kuhakiki taarifa iliyopo kila mahali hivyo zinakosa usahihi wa kutoa majibu sahihi ya uhakiki wao.

Kwa mfano community notes iliyopo twitter X ni bias ina hakiki taarifa zilizo kwenye lugha fulani tu haina data za kutosha kuhusu lugha zingine duniani. Vipi mtu wa Mwanza au wa Kigoma taarifa yake inaweza kuhakikiwa kwa kutumia community notes au fact check kwa kutumia lugha ya maeneo walipo?​
WhatsApp Image 2024-06-07 at 13.29.22.jpeg

Ujio wa teknolojia mpya ya akili mnemba (AI) ndio inaogopesha zaidi taasisi za kimataifa na serikali kwa sababu hizi AI zinauwezo wa ajabu wa kuzalisha maudhui potofu katika meseji, sauti na video na kuzisambaza kwa kasi na viral ni ngumu watu kuzitambua kwa haraka kama ni potofu.

Hapa nchini kwetu matumizi ya teknolojia ya AI bado hayafahamiki vizuri ila kuna uwezekano mkubwa baadhi ya watu kutoka mataifa mengine wakatumia ili kupotosha watu kipindi cha uchaguzi na katika matukio mengine ya nchi.

Sasa kuelekea katika Tanzania tuitakayo wananchi ni lazima wapate taarifa sahihi ili kufanya maamuzi sahihi, hizi ni baadhi tu ya njia ambazo tunaweza kuzitumia ili kupambana na taarifa potofu.​
  • Kwa zama hizi za utitili wa taarifa kila mwananchi anapaswa kujengewa uelewa (skeptical knowing) wa namna bora ya kutambua taarifa potofu na kupambana nazo hivyo kila mwananchi anapaswa kuwa mhariri binafsi wa kila taarifa zinazomfikia na asikubali mtu yeyote kuhariri taarifa kwa ajili yake.​
  • Wananchi wanapaswa kutumia mifumo ya kiteknolojia ya uhakiki wa taarifa (fact check) inayofanyiwa update mara kwa mara na matumiz fact check Zaidi ya moja ili kubaini ukweli wa taarifa fulani maana matumizi ya fact check moja peke yake haiwezi kukupa usahihi wa taarifa.​
  • Kuelekea katika matukio yanayobeba maslai ya umma kama vile uchaguzi wa viongozi ni lazima kufanya pre-debunking ya mambo yanayoweza kupotosha umma ili watu watambue mapema namna ya kupambana na taarifa potofu pindi zinapojitokeza.​
  • Serikali ni lazima sasa watengeneze sera bora ili kupambana na taarifa potofu kuanzia level ya watoto,vijana,wamama,wazee .Pia kuweka miongozo na uwajibikaji kwa wadau wote waliomo katika chain ya kukusanya,kuchakata na kutoa taarifa.​
  • Tunapaswa kupitia upya mitahala ya wanafunzi wanaosoma uandishi wa habari katika vyuo vyote vilivyopo nchini ili kuzalisha wanahabari watakaosaidia kuelimisha umma namna ya kupambana na taarifa potofu katika mifumo ya kiteknolojia.​
Mwisho, kuna mstari mwembamba sana kati ya mapambano dhidi ya taarifa potofu na kuzuia uhuru wa maoni.kilichopo leo duniani ni kwamba maudhui ambayo mtu binafsi hataki kuyasikia basi anaya term kama ni uongo na kuyathibiti. KABLA HUJASAMBAZA TAARIFA YEYOTE NI VYEMA UKAHAKIKISHA KWANZA.

5.jpeg
 
Back
Top Bottom