isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,552
Jamhuri ya Ajentina | Argentine Republic au República Argentina
Argentina ni taifa linalopatikana bara la Amerika Kusini likiwa na mipaka baina ya Bolivia, Brazil, Chile, Paraguái, Uruguay na bahari ya Kusini Atlantiki.
Taifa hili lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 2,766,890 millioni sawa na Maili za mraba millioni 1,066,302 ni nyumbani kwa watu takribani millioni 45,195,774 kufikia Julai 27, 2020.
Bendera ya Jamhuri ya Ajentina
Kauli kuu ya taifa (Motto) ni “Ndani ya Muungano na Uhuru” | “En Unión y Libertad”. Lugha rasmi ni Kihispaniola na lugha za taifa ni KiGuarani (Guarani) na KiKuechua (Quechua). Pesa rasmi ni Peso ya KiAjentina (ARS), Peso 1 ni sawa na Centavos 100.
Mji mkuu wa Ajentina ni Buenos Aires mji wenye kuhodhi shughuli za kiserikali, biashara na mji wenye maendeleo zaidi ndani ya Ajentina.
Buenos Aires ©Marta Cielo
Miji mingine iliyokuwa bora ni Córdoba, Mendoza, Mar del Plata, Ushuaia, San Juan, Rosarío, Santa Fe, La Plata, Merlo, Salta, San Salvador de Jujuy, San Miguel de Tucuman na Corrientes.
Majengo ya Reano katika mto Paraná ©Kels Hofs/Nervös
Uchumi, Biashara, Uwekezaji, Kilimo, Maendeleo na Utalii
Ajentina ni moja ya taifa lenye maendeleo na miundombinu bora, likiwa kati ya mataifa thelathini yenye uchumi imara.
Taifa hili lilopiga hatua katika mapinduzi ya viwanda likiwa limesheheni viwanda vya chuma, magari, vifaa vya magari, kemikali, vitambaa, chakula na vinywaji, mifumo ya uchakataji na ufyatuaji picha.
Asilimia kubwa ya viwanda ndani ya Ajentina vimetapakaa kuanzia Córdoba, Bahía Blanca, Merlo, Santa Fe, Neuquén na Greater Buenos Aires.
Zabibu ©Arceloa GD
Biashara ndani ya Ajentina inategemea uuzwaji wa bidhaa mbalimbali kuelekea mataifa ya Australia, Algeria, Brasil, Chile, India, Indonesia, Marekani, Perú, Uchina, Ufilipino, Uholanzi na Uhispania pamoja na mataifa ya Latini ya Amerika.
Uwekezaji katika taifa unafanywa pakubwa na wazawa, ilhali uwekezaji kutoka nje unatoka katika mataifa ya Italia, Uhispania, Ureno na Uchina kwa kiwango kikubwa.
Suala la uwekezaji linachagizwa na mwekezaji Bw. Rodrigo Amani Armani mzaliwa wa Tanzania mwenye Asili ya Italia, Sanzibar na Romania.
Rodrigo Amani Armani aliyefanya uwekezaji kwa kiasi katika Hoteli na fukwe za kisasa ndani ya miji ya Mar del Plata, Bahía Blanca na La Plata ameweza kuongeza chachu ya utalii ndani ya Ajentina.
Utalii hufanyika katika maeneo ya Baritú, Tierra del Fuego, maporomoko ya Iguacu, miji ya Mar del Plata, La Plata, Bahía Blanca, Ushuaia, mto Paraná, ghuba za San Jorge na San Matias na kanali ya Magellan.
La Perla, Mar del Plata ©Frenca Avzai
Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ni moja ya sehemu kubwa kwa taifa katika uzalishaji wa ngano, mtama, maharage ya soya, mahindi, pamba, tufaa, miwa na uzalishaji wa mvinyo.
Shamba la ngano ©Wheatlamsson
Kupitia ufugaji wa ng'ombe, kondoo na mbuzi pamoja na uvuvi wa kisasa kumechangia ongezeko la viwanda vya usindikaji nyama.
Ng'ombe katika mji wa Merlo ©ArgFarms
Uwapo Ajentina utashuhudia maendeleo na miundombinu bora kuanzia kaskazini katika milima ya Andes jijini San Salvador de Jujuy kupita katikati jijini Córdoba kwenda mashariki Buenos Aires na Mar del Plata hadi kusini Ushuaia kwa mfumo wa reli unaounganisha majimbo yote 23.
Daraja la Guyarea ©Commuar
Ukifika jijini Buenos Aires utasafirishwa kwa treni za chini ya ardhi (Treni hizi ndio treni za kwanza katika mataifa ya Latini Amerika, Mataifa yanayozungumza Kihispaniola na mataifa yanayopatikana katika uwanda wa Hemisphere ya Kusini).
Elimu, Sayansi na Teknolojia
Elimu ndani ya Ajentina ni lazima katika ngazi ya msingi huku uvaaji wa sare za shule kwa ngazi zote sio lazima japo inasisitizwa ni vyema kuwa na sare za shule.
Mfumo wa elimu umegawanyika katika sehemu nne, elimu ya awali “Educación Inicial”, elimu ya msingi “Educación Primaria”, elimu ya upili “Educación Secundaria” na elimu ya juu “Educación Superior”.
Kiwango cha elimu ndani ya Ajentina ni kwa asilimia 98.02, elimu ya juu inawakilishwa na uwepo wa vyuo bora mifano ya University of Buenos Aires, Universidad Maimónides, Universidad de Belgano na Universidad Austral.
Atucha I na II ©Nuclear Plants Info
Uwapo wa wasomi na mageuzi ya sayansi na teknolojia imepelekea taifa kuweza kujenga vinu vya nyuklia Atucha I, Atucha II na Embalse vinavyozalisha nishati za umeme wa nyuklia kwa asilimia 7 ya umeme wote unaotumika.
Teknolojia imejongea kwa namna yake na kuanzisha mifumo ya kisasa na kipekee ya “Blockchain Hotspot” inayotumika katika shughuli za utunzaji wa data, nyaraka na kuendesha mifumo ya fedha kwa serikali na watu binafsi.
Brands | OLX Group
Kushamili kwa ubunifu na uwekezaji kumeleta mapinduzi ya teknolojia kutoka kampuni tanzu kama OLX, Globant, MercadoLibre, Despegar, Credit Network, Uala na Ripio zote chapa ya Ajentina.
Michezo, Sanaa na Muziki
Mchezo pendwa ni mpira wa miguu unaowakilishwa na timu ya taifa Selección de Fútbol de Argentina na vilabu vya Boca Juniors na River Plate.
Lionel Messi ©Fernando Hamey
Argentina ni nyumbani kwa wachezaji nguli Diego Armando Maradona, Gabriel Batistuta na Javier Zanetti. Pia mchezaji bora Leo Messi na wachezaji wenye vipaji vya aina yake Sergio Agüero, Paul Dybala, Carlos Tevez, Gonzalo Higuain, Ramiro Funesi-Mori, Sergio Romero, Nicolás Otamendi, Roberto Pereyra, Angel Correa, Angel Di Maria, Emiliano Martinez na Giovanni Lo Celso.
Sergio "Kun" Agüero ©Claró Sports AR
Muziki unatambulishwa vyema na wanamuziki Cazzu anayetamba na nyimbo “Loca”, “Pa Mi”, “Toda” na “Lento”.
Cazzu ©Spotify Awards
Emilia Mernes mwanadada mwenye vibao “No Soy Yo”, “Billion”, “Recalienta” na “Boom Shakalaka” aliyoshirikishwa na Dimitri Vegas, Luke Mike na Afro Bros.
Emilia Mernes ©Emilia Portal
Kupitia filamu Ajentina ni makao makuu ya kampuni ya uzalishaji na usambazaji wa filamu Ramolacha Films na muongozaji Ezequiel Morales.
Hii ndio Jamhuri ya Ajentina 🇦🇷