Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,814
- 13,580
Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma imesisitiza juu ya umuhimu wa taarifa sahihi katika nyakati ambapo yanaibuka magonjwa mbalimbali ya milipuko nchini.
Akizungumza leo October 4, 2024 katika mafunzo na Wanahabari yaliyoratibiwa na Kitengo Elimu ya Afya kwa Umma kuhusu namna ya kuripoti kwa usahihi magonjwa ya milipuko ya Marburg na Mpox , James Mhilu ambaye ni Afisa kutoka kwenye kitengo hicho, mbobezi wa mafuriko ya taarifa wakati wa milipuko (Infordemic), amesema kukosekana kwa utaratibu wa upatikanaji wa taarifa sahihi umekuwa ukipelekea changamoto yanapotokea magonjwa ya milipuko, ambapo ametolea mfano kipindi cha UVIKO-19 kwamba kulikuwepo na taarifa nyingi za kupotosha.
"Wakati wa matishio ya milipuko ya Magonjwa mbalimbali ni muhimu sana kuwa na mifumo ambayo inaweza kuaminika na Wananchi kwa ajili ya kupokea au kutoa taarifa sahihi." amesema Mihilu
Anaongeza "Tuliona wakati wa UVIKO-19 kwamba kila Mtu alikuwa mtaalamu wa kutoa taarifa, wakati mwingine Watu ambao hata walikuwa sio vyanzo rasmi, waliweza kuaminika na jamii"
Ametolea mfano changamoto ambazo utokana na utoaji wa taarifa zisizo sahihi namna ambayo zinavyoleta mkanganyiko.
"Naweza kutoa mfano, kwa mfano Mganga Mkuu wa Serikali kuna wakati anaweza akatoa taarifa ambazo ni sahihi kabisa, lakini kutokana na Watu wachache ambao wameshapata umaarufu fulani kwenye mitandao, anatoa taarifa ya kupotosha lakini jamii inamuamini zaidi yeye kwa sehemu kubwa. Yote haya ukiangalia ni udhaifu katika namna ambayo Watu wetu wanaweza kupokea taarifa pamoja na kuzichambua au kujua wapi wakapate taarifa sahihi," amesema Mhilu.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo ili kupata muharobaini anasema "Tunaona kuna baadhi ya Watu ambao ni 'Champion' katika masuala ya habari hususani katika Mitandao ya Kijamii, Mfano tunaona kuna chombo kinaitwa JamiiForums wameanzisha kitu kinaitwa JamiiCheck ambapo kama kuna upotoshaji wowote Watu wanatuma taarifa, wao wanaenda kujiridhisha na kutoa taarifa sahihi"
Anaongeza "Huu ni mfumo mzuri ambapo hata sisi Wizara ya Afya tunafikiria kushirikiana nao katika eneo hili la masuala ya magonjwa, kuweza kujifunza namna gani ya kukabiliana na taarifa za uongo na vilevile kujua wapi tunaweza kupata taarifa sahihi na ni Watu gani wanapaswa kuaminika wakati wa dharura za kiafya."
======================
WIZARA YA AFYA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI KUKABILIANA NA UGONJWA WA MPOX NA MARBURG
Leo Oktoba 4, 2024 Wizara ya Afya imetoa mafuzo kwa Waandishi wa habari na Wahariri kutoka vyombo vya habari mbalimbali Nchini kuhusu ugonjwa wa Mpox na Marburg ili kuweza kutoa elimu kwa jamii namna ya kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa hayo.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu amewataka wahariri na waandishi wa habari kutumia taaluma zao kuweza kuifikishia jamii elimu na hamasa juu ya kujikinga na magonjwa hayo ya mlipuko.
"Wanahabari na Wahariri wote tuendelee kushirikiana na Wizara ya Afya na kujenga mahusiano mazuri ili tuweze kuikinga jamii yetu dhidi ya magonjwa haya ya mlipuko, tuelimishe na kuhamasisha jamii kuweza kufuata hatua mbalimbali za kujikinga kama kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kuepuka kushikana mikono na njia nyingine za kujikinga na magonjwa haya", amesema Dkt. Ona
Aidha Dkt. Ona ameitaka jamii kuendelea kujikinga na kuchukua tahadhari zote muhimu ili kujikinga na magonjwa hayo kwani tayari baadhi ya nchi za jirani zina maambukizi ya magonjwa hayo.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Afya Bw. Englibert Kayombo amesema kuwa semina hiyo ya waandishi wa habari ni endelevu na taratibu za Wizara kukaa pamoja na wadau hao ili kuwapa elimu muhimu itayawasaidia katika kutoa taarifa kwa usahihi.
Naye James Mhilu, Mratibu wa Mafunzo hayo amewataka Waandishi wa habari na Wahariri kuwakumbusha wananchi kupiga namba 199 kituo cha miito ya simu cha Wizara ya Afya (Afya Call Center) kwa taarifa, maoni na ushauri zaidi.
Semina hii kwa wanahabari ni jitihada mojawapo zinazochukuliwa na Wizara ya Afya katika kufikia jamii kupitia waandishi wa habari ambao sasa wamewezeshwa na elimu muhimu kuhusu magonjwa ya Mpox na Marburg.
Chanzo: Wizara ya Afya