Sikumbuki ni lini sijaacha kuvutiwa na aina yake uwasilishaji wa hoja mbele ya jamii pale anapokuwa anazungumza. Japokuwa Mheshimiwa Mbunge huyu wa Vunjo James Mbatia tunatofautiana katika ITIKADI tu za Vyama vya Kisiasa ila huyu jamaa hakika ni Hazina tosha kwa Maendeleo ya sekta mbalimbali kwa nchi hii kwa UHODARI wake wa KUTUKUKA.
Hoja yangu kubwa ya leo ni kutaka tu kusema kuwa Mbunge James Mbatia hakika anatuonyesha kuwa kusoma siyo kuwa na Cheti bali kusoma ni kuitumia ile elimu yako uliyoipata huko Chuo Kikuu na kuleta TIJA kwa nchi yako au jamii inayokuzunguka.
Nisifiche na hili najua litawauma wengi ila kama kawaida yangu huwa napenda kumpa mtu haki yake iwe ni katika KUMKOSOA au KUMSIFIA yote ikiwa ni katika kujengana na tuwe vizuri. Nina uhakika kuwa karibu 85% wa Wasomi wa Tanzania waliopita Chuo Kikuu kipaumbele chao kilikuwa ni kupata tu Degree au Masters au PhD na ni Watanzania wachache sana kama hiyo 15% iliyobaki ambao wamekwenda Vyuo Vikuu kusoma, kuelewa na kuja kutumia ile elimu yao kwa jamii.
Mbunge James Mbatia ANATUUMBUA wengi sana tunaojiita INTELLECTUALS au ACADEMICIANS na huyu jamaa nina uhakika kuwa kama angekuwa anaishi nchi za wenzetu wanaojua kuthamini michango ya Watu basi mpaka leo angekuwa na hata TUZO 50 za EULEDI wa masuala mbalimbali.
James Mbatia ni mtu ambaye hata kama ukiwa unamsikiliza katika redio au unamtizama katika runinga basi utatamani muda wote awe tu anaendelea kuzungumza na kutoa UFAFANUZI wa jambo lililopo mbele. Mheshimiwa Mbunge James Mbatia japo mimi ni Mwana CCM tena wa KINDAKINDAKI naomba ruhusa yako kuanzia leo nikubatize nikuite PHILOSOPHER AND GREAT THINKER OF ALL THE TIME.
Sifa zako hizi zifuatazo zimenifanya nishikwe na aibu na leo nijitokeze na kiseme ukweli wangu kwako kuwa mimi ni mmoja wa wale WANAOKUKUBALI kwa 100% bila kujali Siasa zetu:
- Buoyancy.
- Scholarly.
- Prescient.
- Talented Orator.
- Intrepid.
- Prognosticator.
- Xenophobic.
Mheshimiwa Mbunge James Mbatia naomba usiache kusema yale unayoyaamini ili uje kuacha historia yako ambayo itakumbukukwa na vizazi na vizazi na labda nitoe wito tu kwa Wasomi wengine hebu jaribuni kuwa kama Mbatia ambaye ametuonyesha kuwa hakwenda University kutafuta tu Cheti kisha aje atambe nacho huku mitaani kama ambavyo Wasomi wengi walivyo bali alikwenda Chuo Kikuu kupata MAARIFA na UJUZI.
Tunahitaji aina ya elimu ambayo imemjenga hivi alivyo Mheshimiwa Mbunge James Mbatia ambayo ni elimu ya kumfanya mtu awe na ueledi wa kweli katika fani fulani au kile anachokisimamia na Tanzania ya sasa hatuhitaji elimu ya kujaza vyeti ukutani au chumbani wakati kichwani ni POPOMA mtupu na huna msaada wowote si tu kwako au kwa jamii yako bali hata kwa taifa letu zima.