- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Jaji Joseph Sinde Warioba alikuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Novemba 5, 1985 hadi Novemba 9, 1990. Pia ni Mwanasheria, Mwanasiasa na Jaji maarufu anayeheshimika Kitaifa na Kimataifa kwa mchango wake mkubwa katika masuala ya Sheria na Utawala Bora.
Warioba ni miongoni mwa wakosoaji dhidi ya ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia na haki za binadamu ambaye mara kadhaa amekuwa akihusishwa na taarifa potoshi ambazo zimekuwa zikitengenezwa ili kupotosha umma. Rejea hapa.
Kumekuwapo na machapisho yanayosambazwa kwa pamoja mtandaoni yakiwa na madai mbalimbali ikiwemo ‘Jaji Warioba kuungana na Lissu, CHADEMA kuikacha CCM, vita Urais, kanisa katoliki kuwatumia Gwajima, Mpina kugombea urais kupitia CHADEMA, machapisho yakidaiwa kutolewa na Jambo TV huku chapisho lililodaiwa kuchapishwa na The Chanzo likiwa na kichwa cha habari “mpango wa warioba kuipinga CCM wavuja: siku chache baada ya Lissu kuongea atatoka hadharani”
Je, uhalisia wa machapisho hayo ni upi?
Chapisho lililodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ‘Jaji Warioba kuungana na Lissu, CHADEMA na kuikacha CCM’
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na Jamiicheck kwa kutumia key word search ulibaini kuwa kurasa rasmi za mitandao za Jambo TV hazikuchapisha taarifa hiyo. Pia chapisho limebainika kuwa na mapungufu yanayolitofautisha na machapisho rasmi ya televisheni hiyo ya mtandaoni, matumizi ya mwandiko (fonts) ambao hautumiwi na Jambo TV, ubora mdogo wa muonekano wa grafiki ambayo imetumika kutengeneza taarifa hiyo ni sehemu ya mapungufu hayo.
Kadhalika chapisho lililohusisha kanisa katoloki kuwatumia Gwajima, Mpina kugombea Urais kupitia CHADEMA si la kweli kwani halikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za televisheni hiyo. Pia mwandiko (fonts) uliotumika katika chapisho hilo ni tofauti na ule unaaotumiwa katika machapisho rasmi. Hata hivyo picha inayoonesha kuwa Emmanuel Ntobi aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga kuwa alichapisha chapisho hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X si kweli kwani Tarehe 10, Februari 2025 ukurasa huo haukuchapisha taarifa hiyo.
Chapisho lililodaiwa kuchapishwa na The Chanzo likiwa na madai ‘mpango wa Warioba Kuipinga CCM wavuja’
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa Chapisho hilo si la kweli na halikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za The Chanzo. Hata hivyo chapisho hilo lina mapungufu yanayolitofautisha na machapisho halisi ambayo huchapishwa na The Chanzo, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kukosekana kwa tarehe husika ya taarifa kuchapishwa kama ambavyo inatumiwa katika machapisho rasmi, pia kutofautiana kwa mwandiko (fonts)ambao umetumiwa katika chapisho hilo ni tofauti na unaotumiwa katika machapisho rasmi.