Uchaguzi 2020 Jamani, ruzuku ni tamu; Msitegemee hawa watu kuungana

abdulhamis

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
1,436
2,293
Habari wadau,

Nimeona niseme jambo kuwa vyama vya upinzani Tanzania vyote vipo kimaslahi zaidi; hamna chama kipo ili kimtumikie mwananchi.

Na kama kweli wapo ili kumtumikia mwananchi kwa yale wanayosema kuwa wanachi tunaibiwa na kufanywa kuwa maskini na CCM hivyo lazima tuitoe madarakani, basi waanze kwanza wao kutokua na Uroho wa Madaraka na kuchumia matumbo yao, yaani ajenda iwe ukombozi na sio Ruzuku.

Chama cha CHADEMA na ACT haviwezi kuungana bila kukubaliana maslahi kwanza.

Pili kuna kiongozi wa CHADEMA yeye yuko tayari kumsapoti ACT katika Urais ila yeye abaki na wabunge wengi sababu anajua kushinda urais si kweli, hivyo yeye anataka chama kibaki kuwa na nguvu, hivyo usishangae kama kweli CHADEMA na ACT wataungana basi mjue tu kauli Itakua "Tunaenda na Membe"

Hapo ndio Msingida Atakapo changanyikiwa. Tujipe Muda.
 
Siyo ruzuku. Ni mambo ya itikadi.

Hivi kama ungelikuwa wewe ungeungana tu bila kufanya nchanganuo?

Hakuna Mtanzania mwenye nia njema ama mwenye ufahamu ataongea habari za membe kuwa raisi. Akisimamishwa membe, hatuna sababu ya kumtoa Magufuli Madarakani. Kwanza CCM ya Magufuli iko mashariki sana kuliko ile ya kina Membe. Membe ana sifa gani ya kufanya hata awe balozi wa nyumba kumi?

Naomba tutumie jukwaa vizuri.
 
ACT ni janja janja wanataka wapate kote, anaweza kuwa mshirika mzuri ila sio wa kuaminika.

CHADEMA wawe makini ikibidi hata kutokuwa na ushirikiano kabisa, haiwezi kidhuru Lissu bado no brand kubwa
 
ACT ni janja janja wanataka wapate kote, anaweza kuwa mshirika mzuri ila sio wa kuaminika.

CHADEMA wawe makini ikibidi hata kutokuwa na ushirikiano kabisa, haiwezi kidhuru Lissu bado no brand kubwa
Kwa uzoefu wa matukio cdm ndio janja janja tena sio ya kuaminika ref; walivyogawana majimb kipind cha ukawa na walichokifanya
 
Lisu anaupepo mkali vibaya mno hata asimame nani hawezi kuzuia upepo wa Lisu yule membe wananchi wanamshitukia kua luwasa mungine upinzani ndio maana hato fua dafu kwa Ni yeye 2020
 
Kwa Membe hapana, itakuwa kama Lowasa, na pia kampeni zitakuwa ngumu sana tofauti na Lissu(The guy is clean). Wanajaribu kumchafua Lissu na propaganda sijui za ushoga mara sio mzalendo anaisema nchi vibaya huko nje, lakini hawana hoja.
Wakitaka tuwachambue vizuri, iwekwe debate kati yao watatu tuwapime, pia kuwe na fair ground kwenye uchaguzi(uwe huru na wa haki + kuwe na uwazi) sio kuficha ficha kwenye kuhesabu kura utadhani mgombea atagundua mwandiko wako kwamba umempigia fulani badala yake. Hapo ndipo utaona tofauti ya maji na mafuta.
 

From 48 Laws of Power...."win actions, not words". A silent fool is considered wise.
Waonyeshe watu SGR, siyo ILANI ya uchaguzi ya chama
 
Kwanini hamuiongelei TLP au CUF au UDP , DP viungane?! Kama kweli umoja ni nguvu, nataka nione TADEA, PONA, CCJ, TPP, UDP, TLP, demokrasia Makini, viungane hata uwaongese na ACT na NCCR humo.

Vipewe support yote tuone kama vitapata hata diwani mmoja?!

Zitro na ACT wanaweza Zanzibar tu, NCCR hawajui waanzie wapi, CUF wao wanagombea buguruni, sijui kwanini mnadhani vitaisaidia CHADEMA .!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…