Jamani mwenzenu siwezi kuacha kabisa.

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
8,626
13,847
Nikianza kusema hivyo kuna watu watafikiria kuna kitu nafanya halafu siwezi kuacha kukifanya.Sio hivyo mimi siwezi kuacha kwa maana ya kuacha hasa.

Mimi kwa sasa nimebaki na wake watatu baada ya mmoja kutangulia mbele ya safari..Hawa wake zangu si malaika kama nilivyo mimi,huwa kuna siku wananiudhi sana mpaka nakasirika.Pamoja na hivyo maudhiko yangu hayanipelekei kufikiria kumuacha yoyote kati yao.

Iko siku mmoja alinichokonoa kwa kurudia shutuma hiyo kwa hiyo.Nikiingia hadhithi ni hiyo,nikianza kula hadithi ndio hiyo hiyo.Nikiingia ndani kulala mambo ni hayo hayo.Siku iliyofuata akasubiri mpaka ndugu zake wamekuja kumtembelea akanizodoa kwa uzushi ule ule.Loo ! nikajitkuta imenitoka "Nimekuacha.talaka si mke wangu".

Kama unavyojua kwetu waislamu talaka ni halali inayomchukiza sana Mwenyezi Mungu na vile vile huwa hakuna utani katika tamko la talaka ulilotoa.Ukitamka tu hata kwa utani limeshatimia inabaki hesabu tu ni mara ya ngapi na ikifika mara ya tatu hakuna dawa ila mke kama unamtaka aolewe na mume mwengine walalae na wafanye halafu huyo mume aje amuache kwa hiyari yake ndipo kama unamtaka tena uweze kumuoa wewe wa awali.

Turudi kwenye mada kuu.Siku hiyo baada ya kutamka talaka nikaona maajabu mwenyewe na waliokuwepo badala ya aliyeachwa kushtuka,mimi ndiye niliyepatwa na huzuni kubwa na nikalia kwa kwiki kuliko watoto wetu.
Simanzi zikanifanya kujionea aibu na nikaingia chumbani kwa mke wangu na ikawa nimeshamrudia.Kuna fikra za kihistoria za wema aliowahi kunifanyia na furaha wakati tukiwa hatuna ugomvi na subira yake wakati wa shida

Baada ya hapo sifikirii tena kutoa tamko hilo.Na si kwamba sifikirii tu bali siwezi kabisa.Vinavyonishinda kutoa talaka au kuwa mbali na wake zangu na hivi vifuatavyo

1.Mimi naamini kuwa wanawake wote bila mume ni maskini sana na wanatia huruma sana.Hivyo sitaki mke wangu aingie kwenye kundi hilo

2.Mwanamke hata akiwa tajiri wa mali ni maskini sana bila kupata mume wa kuwa naye karibu ama kutumia hizio pesa au kama hana lazima atumie za mume wake na hawezi kupata pesa nyengine bila kudhalilikia mbele ya wanaume wengine.Sipendi kabisa mke wangu baada ya raha aje apate hali hiyo.

3.Napata wivu mkali nikiwa mbali na mke wangu kwa kunijia fikra kuwa kwa vile mwanamke hawezi kukaa bila mume basi akiwa mbali na mimi kuna mwanamume mwengine atajikaribisha naye halafu aonje vile vilivyoniburudisha mimi

4.Hiyo namba tatu inakaziwa na pale mke wangu anapokuwa amesafiri kwenda mbali hasa nje ya nchi.Kila wakati huwa nahisi ana mahitaji ambayo inabidi nimtimizie kwa haraka.
Iko siku mke wangu alisafiri kwenda mbali na mimi.Alipofika huko akakuta hali ya maisha ni ngumu sana na akawa ananisimulia hali zilivyo na kwamba pesa zilikuwa zimemuishia.Njia zote za kumfikishia matumizi zikawa ngumu kwa siku mbili mfululizo.
Nikajikuta napata maumivu ya hali yake na nikawa nalia tu.Nikaona kama mke wangu ananyong'onyea kwa njaa na anakaribia kuanguka.Nikakisia pamoja na hali mbaya za maisha za mji huo lakini wanaume wa kule ni matajiri sana na wanaweza wakamuona mke wangu anavyohaha kwa njaa na kukosa matumizi halafu wakaanza kumsaidia wakitaraji kupata fadhila kutoka kwake.

5.Kila pale mke wangu anapoumwa huhisi kama ndio anakufa siku hiyo.Nikikumbuka upweke nitakaokuwa nao akiwa hayupo huanza kulia japo yuko hai.

Vitu vyote hivyo vimenifanya niielewe vizuri ile hekima ya Mwenyezi Mungu aliposema
ﻭَﻣِﻦْ ﺁﻳَﺎﺗِﻪِ ﺃَﻥْ ﺧَﻠَﻖَ ﻟَﻜُﻢ ﻣِّﻦْ ﺃَﻧﻔُﺴِﻜُﻢْ ﺃَﺯْﻭَﺍﺟًﺎ ﻟِّﺘَﺴْﻜُﻨُﻮﺍ
ﺇِﻟَﻴْﻬَﺎ ﻭَﺟَﻌَﻞَ ﺑَﻴْﻨَﻜُﻢ ﻣَّﻮَﺩَّﺓً ﻭَﺭَﺣْﻤَﺔ ًﺇِﻥَّ ﻓِﻲ ﺫَﻟِﻚَ ﻟَﺂ ﻟِّﻘَﻮْﻡٍ ﻳَﺘَﻔَﻜَّﺮُﻭﻥَ ﻳَﺎﺕٍ
“Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.” [Ar-Ruum 30: 21]
 
Samahani bro!!!Kwahiyo yule shemeji yetu uliyemtamkia umemuacha ilibidi atafunwe kwanza ndio ukamrudia?
Mambo mengine mazito kwelikweli.
Siyo hivyo. Hiyo kitu inakuwa lazima kama kwa hasira zako utakuwa unatamka tamka mpaka inafikia mara tatu.
Kwa mara ya mwanzo na ya pili ni wewe tu.Ukiamua hapo hapo inakuwa imeisha.
 
Samahani bro!!!Kwahiyo yule shemeji yetu uliyemtamkia umemuacha ilibidi atafunwe kwanza ndio ukamrudia?
Mambo mengine mazito kwelikweli.
Nilishaona nadhani kwenye movie ya ray, jamaa alimpa mwanamke talaka tatu lkn baadae akaona bado anampenda, ili kuweza kumrudia tena ikabidi wakae chini na huyo alokua mke wake wakubaliane mke wake akaolewe na rafiki yake kisha rafiki yake aje kumuacha baadae. Lakini alooooh, shimo likanasa mpini, na mpini ukakubali kutotoka, mke akaenda kwa jamaa mazima, jamaa akaona bora avunje urafiki ila sio kuacha kile chombo.Mwamba akabaki analia lia tu. Ila kama wewe ni mwanaume halisi huwezi kukosa msimamo mara uache, mara urudie hizo ni tabia za kike
 
Nilishaona nadhani kwenye movie ya ray, jamaa alimpa mwanamke talaka tatu lkn baadae akaona bado anampenda, ili kuweza kumrudia tena ikabidi wakae chini na huyo alokua mke wake wakubaliane mke wake akaolewe na rafiki yake kisha rafiki yake aje kumuacha baadae. Lakini alooooh, shimo likanasa mpini, na mpini ukakubali kutotoka, mke akaenda kwa jamaa mazima, jamaa akaona bora avunje urafiki ila sio kuacha kile chombo.Mwamba akabaki analia lia tu. Ila kama wewe ni mwanaume halisi huwezi kukosa msimamo mara uache, mara urudie hizo ni tabia za kike
Inauma sana kulazimisha aolewe halafu umrudie.Ni adhabu nzuri sana kwa wanaume wasio na uvumilivu wa tabia za kike.
Jirani yangu alifanyiwa kama hivyo baada ya mke wake kumuacha mara tatu.Siku moja nikamuona ustadhi fulani asubuhi anatoka kwenye ile nyumba yule dada kajipamba vizuri akampakia anampeleka kwa baba yake kwamba yeye keshamaliza kazi.Roho iliniuma sana. yule bwege baadae akamrudia na ndio wamepata watoto kadhaa.Mimi bado namuhurumia sana nikijua mimi siwezi hiyo.
 
Back
Top Bottom