Jamani mimi mapenzi tena basi!

Mfalme Akili

Member
May 28, 2017
88
55
Habari za mwezi mtukufu wa ramadani!
Mimi ni mgeni humu jamii forums lakini nahisi nyinyi ni watu wenye upendo na ushauri mzuri basi naombeni ushauri wenu.

Sijui nina kasoro gani maana kila ninapopenda natendwa, sijui ni kwanini kwa sababu ninadhani ninavyo almost vitu vyote ambavyo mabinti au wanawake hupenda kwa mwanaume, lakini nashangaa kila mwanamke nimpendae mwisho wa siku huishia kunitenda, kama sio kuniacha basi atanisaliti.

Ngoja kwanza nitoe wasifu wangu, mimi ni kijana wa makamo nina miaka 27 kwa sasa, nina kazi nzuri inayonilipa vizuri mbali na hapo nina biashara zangu binafsi za nyumba na viwanja (real estates) zinazoniingizia si chini ya laki 5 kwa siku namshukuru mungu pesa ya kubadili mboga na mafuta ya gari haisumbui.

Pia nimebahatika kupata nafasi ya kuhudhuria gym kila siku tano za wiki hivyo mwili wangu unaonekana vyema na pia sura yangu si nzuri wala si mbaya nadhani nipo kwenye kundi la watu wa kawaida ki mtazamo wa sura.

Ukija katika upande wa uanaume ki ukweli namshukuru mungu kanijalia mtarimbo wa maana na show napiga ya uhakika siyo kwamba najisifia ila huo ndo ukweli halisi, kiufupi bao la kwanza hua hata sipumziki naunganisha, (hapo kama nimeenda kavu na binti ninae muamini kiafya). Na kila binti niliyewai kushiriki nae tendo la ndoa hudhihirisha dhahiri ufundi wangu katika shughuli hiyo.

Lakini cha ajabu nimekua mtu wa nuksi kila binti ninaeamua kua nae katika uhusiano mwisho wa siku huishia kuniacha au kunisaliti (Kunicheat) najiuliza why? coz ninampa kila anachohitaji kuanzia mapenzi mpaka basic needs n.k.

kilichofanya niandike waraka huu ni binti niliyempata mwaka jana mwezi november ambaye alikua tofauti na wengi walionisaliti, yeye alionekana innocent sana kuanzia sura mpaka matendo basi nikasema asante mungu baada ya kusalitiwa na wanawake kama kumi hatimaye umenipa binti wa ndoto zangu. Yani akaichukua akili yangu akanifanya nimuamini kupita maelezo, na wiki mbili zilizopita nimetoka kumtolea mahari baada ya kupata ujauzito.

Lakini navyoandika huu ujumbe kwa sasa ni hivi binti huyo nimemfumania live akiwa na tauro tu na njemba jingine kwenye nyumba jirani hapa mtaani kwetu kwa msaada wa wasamaria wema, kiukweli niliishiwa nguvu na mpaka sasa navyoandika sijui nifanye nini maana hata wazazi wa pande zote mbili sijawaeleza kilichotokea na binti analia muda wote anaomba nimsamahe lakini moyo wangu umekua mgumu kumsamehe roho inaniuma sana na nimeanza kupata mashaka uenda mimba siyo yangu.

Sasa hapa nilipo nimechanganykiwa nimenunua mapombe makali ndiyo nakunywa 24 hours sijui nifanye nini naumia sana na binti huyu kiukweli nampenda sana, ndipo nilipomshirikisha rafiki yangu mmoja ndo akanielekeza nije huku jamii forums uenda nikapata njia.

Jamani naombeni ushauri wenu coz nahisi kufa kufa hivi..!
 
Kwanza wewe ni kijana mdogo Sana, Mungu amekupa mafanikio makubwa. Mshukuru Mungu, omba sana yamkini una mapungufu mengineyo hujijui.
Jaribu kuangalia wapi unakosea jirekebishe, halafu mwambie Mungu unahitaji mke, sio demu tena.
 
Kwanza wewe ni kijana mdogo Sana, Mungu amekupa mafanikio makubwa. Mshukuru Mungu, omba sana yamkini una mapungufu mengineyo hujijui.
Jaribu kuangalia wapi unakosea jirekebishe, halafu mwambie Mungu unahitaji mke, sio demu tena.
Nimeshajiuliza sana wapi nakosea? ila nakushakuru sana ndugu yangu namuomba mungu kila siku, yani angekua hajapata mimba hata nisingewaza sana.
 
Kila mtu kapata torture ya kusalitiwa ndo maisha yalivyo hususani upnde huu tata wa mapenzi, ni kheri umegundua unasalitiwa kabla ya ndoa chamsingi kwa sasa piga chini rudi kundini kwa muda.
 
Jipe breki kwanza jikeep busy na mishe zako usisahau kumshirikisha Mungu kuhusiana na swala lako

Ni mapito tu hizo pombe usinywe tena maana hazisaidii kitu

Ni swala la muda kila kitu kitakua sawa tu kwa muda sahihi uliopangiwa
Nashukuru ndugu, napenda sana mziki basi nisipokunywa pombe bora nisikilize mziki, na wimbo wa lavalava "bora tuachane" ndio unaonipendeza kwa sasa.
 
Kila mtu kapata torture ya kusalitiwa ndo maisha yalivyo hususani upnde huu tata wa mapenzi, ni kheri umegundua unasalitiwa kabla ya ndoa chamsingi kwa sasa piga chini rudi kundini kwa muda.
Asante ndugu, but kuhusu ujauzito alionao mnanishauri vipi?
 
"Something is wrong somewhere" haiwezekani uwe unasalitiwa na kila mwanamke unayempata. Kuna kitu kwako hakiko sawa kwenye sekta ya mapenzi,watafute hao wanawake waliokusaliti uwaulize sababu za usaliti wao nini. Ila uende friendly,utapata jawabu.
 
"Something is wrong somewhere" haiwezekani uwe unasalitiwa na kila mwanamke unayempata. Kuna kitu kwako hakiko sawa kwenye sekta ya mapenzi,watafute hao wanawake waliokusaliti uwaulize sababu za usaliti wao nini. Ila uende friendly,utapata jawabu.
Shukrani ndugu nitafanya ivyo.
 
Kuna rafiki yangu mmoja aliachwa na mpenzi wake akaona njia moja ya kumliwaza ni kunywa pombe mwisho wake kawa teja la nguvu. Kunywa Pombe sio kutatua tatizo lako bali angalia wapi unapo kosea, Hata timu ya mpira inaweza kuwa na wachezaji wazuri na kocha mzuri lakini ikatokea kufungwa na timu pinzani sababu ndio mchezo. Kuna kupata na kukosa kama wanawake wako unawapata kwenye social media,Club,Bar na Gym, basi tafuta njia nyengine ya kutafuta mwenza lakini kama michepuko hizo ndio sehemu zao. Bila ya kusahau unapopata mwanamke usimwambie kipato chako(kuwa una hela) jifanye mtu wa kawaida tu siku za mwanzo panda mwendokasi kumfata. Jitahidi kuwa
1 Mkweli na mwenye confidence
2 Mcheshi ukiwa na mpz wako
3 Kuwa na lugha nzuri ukiwa nae
4 Muulize nini anapenda na nini hapendi
5 Mchunguze bila ya yeye kujua kama unamchunguza nyendo zake.

Kuhusu nini cha kufanya baada ya kumfuma mpz wako na njemba nyengine huo ni uamuzi wa moyo wako, Dalili za mvua ni manyunyu leo imenyesha nje ya ndoa kesho itanyesha ndani ya ndoa. nategemea umenipata kila la kheri mkuu
 
Pole kijana, nakushauri kwa sasa usimwache ama kutangaza kumwacha, tens usiseme hats kwa ndugu, endelea kuwa nae ila kama rafiki bila yeye kujua nia yako, na nia iwe kusubiria had mtoto azaliwe, ili kama so wako basi utaamua kumwacha. Ila nia ya pili iwe kumpa mda ajutie dhambi, nakuhakikishia kipindi hiki had I anajifungua atajutia na kujirekebusha, kumbuka wakati huo ajui mpango wako HVO atatafuta kila hali abadilike na kukuthibitishia. Sasa iwapo yote mawili yatakuwa positive yaani mtoto wako na yeye katubu, baso waweza kumwoa mlee motto. Ila kama mtoto so wako basis hip utakuwa muda mzuri kumwacha na kushirikisha familia. TAMBUA itakuwa aibu sana ukimtangaza kwa familia na kumwacha, ikitokea mtoto no wako itakuwa ngumu kumpata au kumkaribia. Vumilia na mwombe mungu kwa hekima zaidi ! Usikate tamaa, mshukuru mungu hats kwa hili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…