Mimi narudia si mwana CCM, si mwana CHADEMA, si mwana CUF wala hata ACT nk, ni mtanzania halisi, mzalendo. Siipendi CCM na naichukia kama ... kwa sababu tu walivyo fumbia macho maovu na kutufikisha hapa tulipo kama wananchi. Na huwa nawashangaa na kuto walelewa watanzania wengi wanao shabikia CCM na kubaki nimeduwaa.
Aidha, nilihisi Rais Magufuli atakuwa tofauti, ingawa si rahisi kujitoa ama kuichukia kama niichukuavyo mimi, lakini sisi wote ni watanzania na nimefurahishwa na juhudi zake na wakati mwingine hata kuelewa na kukubali hata mimi labda ningepigana vivyo hivyo. A fight from within.
Lakini sasa swali kubwa linalo taka jibu ni hili. Hivi Rais Magufuli atatumbua maipu yote haya bila kugusa kiini cha majipu yaani kimeo chake ambaye ni KIKWETE. Haingi akilini kusimamisha, wakurugenzi, makatibu wakuu, maafisa waandamizi, mawaziri nk bila kumgusa Rais mstaafu kwa namna moja ama nyingine!