Jamani hivi nini kinasababisha mtoto mchanga kutokwa na damu puani na mdomoni na hatimae kupoteza maisha? (Kufariki)

Jamani hivi nini kinasababisha mtoto mchanga kutokwa na damu puani na mdomoni na hatimae kupoteza maisha? (Kufariki).

Pole,

Ingawa neno mchanga halitoi mwangaza mzuri wa umri ili kutoa picha pana zaidi na mazingira ya tukio husika.

Kwa wataalamu wa afya hii huwa ni dalili ya kubanwa kwa mfumo wa hewa/Suffocation. Hupelekea kutoka damu kwenye mfumo wa hewa/mapafu.

Pia huweza kuwatokea watoto waliozaliwa na uzito mdogo au kabla ya umri halisi wa ujauzito.

Hili pia huweza kutokea tunapowalaza watoto na vitu laini vingi kuwazunguka kama blanketi laini nk.

Hali hii kufikiriwa ni pale mtoto mwenye afya njema hubadilika ghafla na kupoteza maisha hasa akiwa ameachwa peke yake amelala au mazingira tatanishi. Hali hii huitwa Sudden Infant Death Syndrome (SIDS).

Ingawa inahitaji maelezo mengi binafsi toka kwako ili kujenga hoja zaidi.

NB: Hapa ndo ushauri wa mtoto ambaye hajaweza kunyanyua kichwa chake vyema/poor or no neck control. HUSHAURIWI KUMLAZA KWA TUMBO AU KIFUDIFUDI.
 
Alianza kulia tu wakati wa usiku, mama yake akawa anamnyonyesha anakitulia baadae ananza tena kulia, imefika saa 11 alfajiri mtoto akaanza kama kupiga chafya, kapiga chafya ya kwanza, alipopiga chafya mara ya pili tu damu zikamtoka puani na mdomoni, tunaenda Hospital tunafika mtoto akiwa ameshafariki teyari, niliumia sana mpaka sasa hivi nashindwa nianzie wapi japo nimeshapata ushauri tofauti tofauti kutoka kwa wataalamu wa afya lakini bado naona sijapata njia sahihi kwakweli.
 
Pole sana.
Umri wake?
 
Alikuwa anasiku 3 tu toka azaliwe, samahani nilikuwa nipo sehemu ambayo hakuna Internet kwa wiki 2 hivi ndo maana nimechelewa kujibu, nilikuwa kwa babu kijijini

Pole sana,

Kwa siku tatu changamoto ni nyingi, ingawa ni theories, jibu sahii lingepatikana kwa kupimwa mtoto/marehemu.
Nitataja vitu vitavyotusiadia ili kujifunza na kikubwa hapa ni ukosefu wa hewa/suffocation.

Mambo yanayoweza kuhusishwa:

1: Mtoto kuzaliwa akiwa na matatito/congenital anomalies kwenye njia ya chakula/mapafu au moyo.

2: Mtoto kunyonyeshwa na kulazwa mara tu baada ya kunyonyesha/milk suffocation. Hasa kwa wazazi wapya/uzao wa kwanza na unyonyeshaji wa usiku au umechoka.

3: Mama kunyonyesha na kushikwa usingizi au umechoka/kwa wale wenye maziwa makubwa/breast suffocation.

4: kumlaza mtoto kifudifudi wakati hajaweza kukaza shingo au kunyanyua kichwa chake/sudden infant death syndrome(SIDS).

5: Kumlaza mtoto mchanga na vitu vingi kitandani kama nguo za kumfunika/SIDS.

6: Kulala na mtoto mchanga kitandani bila tahadhari kwa kuwa na eneo dogo/uwezo wa kumlalia mtoto UKIWA usingizini/SIDS.

NB: Ni vyema kuwa makini katika haya yote wakati wa malezi.
 
Sawa kaka, ila ni mara ya 3 sasa hii, na sina mtoto bado toka 2019 tunapata mtoto anakaa siku 3 hadi 7 anafariki, yaani kama mkosi hivi aisee 😭😭
 
Sawa kaka, ila ni mara ya 3 sasa hii, na sina mtoto bado toka 2019 tunapata mtoto anakaa siku 3 hadi 7 anafariki, yaani kama mkosi hivi aisee
Nendeni muhimbili kwa maspesholist, Kuna mdada alikuwa na tatizo kila akizaa watoto wanakufa wachanga alitibiwa muhimbili na Sasa hivi watoto wakubwa tu.
 
Sawa kaka, ila ni mara ya 3 sasa hii, na sina mtoto bado toka 2019 tunapata mtoto anakaa siku 3 hadi 7 anafariki, yaani kama mkosi hivi aisee 😭😭
Pole sana kaka ila nina swali moja mlishapimaga magroup yenu ya damu wewe na mkeo?
 
Back
Top Bottom