Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,529
Mji mkuu wa Indonesia Jakarta ni nyumbani kwa watu milioni 10 lakini mji huo pia unazama kwa kasi zaidi duniani. Ikiwa hatua hazitachukuliwa sehemu za mji huo mkubwa huenda zikazama kabisa ifikapo mwaka 2050 kwa mujibu wa watafiti.
Mji huo uko eneo lenye kinamasi kando mwa bahari, huku mito 13 ikipita kwenye mji huo na hivyo sio jambo la kushangaza kuwa mafuriko ni jambo la kawaida mjini Jakarta kwa mujibu wa wataalamu, hali inayozidi kuwa mbaya na mji huo ukizidi kutoweka.
Heri Andreas anaonyesha ukuta uliojengwa kuzuia maji ya bahari kufurika nyumba
Tayari inafanyika – eneo la Kaskazini mwa Jakarta limezama mita 2.5 katika kipindi cha 10 na linazidi kuzama kwa karibu sintimita 25 kwa mwaka sehemu zingine. Jakarta huzama kwa kasi ya sentimita 1-15 kwa mwaka na karibu nusu ya mji uko chini ya bahari. Athari tayari zimeonekana Kaskazini mwa Jakarta. Kwenye wilaya ya Muara Baru, jengo lote la ofisi limebaki mahame. Awali ilikuwa ni kampuni ya uvuvi lakini ghorofa ya kwanza ndiyo tu inaweza kutumiwa.
Sehemu ya kwanza sasa imebaki kufurika maji. Ardhi inayozunguka iko juu kwa hivyo maji hayawezi kutoka.
Kuzama kwa mji wa Jakarta kumetokana na kutumika kwa maji wa chini ya ardhi kupitia uchimbaji visima kwa kunywa, kuoga na matumizi mengine ya kila siku miongoni mwa wakaazi wa mji. Maji ya mifereji hayapatikani sehemu zingine kwa hivyo watu hawana lingine ila kutafuta maji mbali zaidi chini ya ardhi.
Manispaa moja hivi karibuni ilikiri kuwa visima haramu vimekuwa tatizo. Mwezi Mei mamlaka za mji wa Jakarta zilikagua majengo 80 kati kati mwa Jakarta, mtaa wa Jalan Thamrin kwenye majengo marefu, maduka na mahoteli. Iligundua kuwa majengo 56 yana visima vyao na 33 yalifanya hivyo bila vibali. Mamlaka pia zinamatumani kuwa Great Garuda, ukuta wa umbali wa kilomita 32 unaojengwa Jakarta utasaidia kuukoa mji huo kuzama kwa gharama ya dola bilioni 40.