chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,071
- 27,187
Nadhani kuna haja ya Mahakama kufanya tathimini katika hili jambo. Majaji wengi hawaandiki hukumu kwa mkono wao na fikra zao binafsi, wanaandikiwa hukumu!
Ukifanikiwa kumjua anayemuandikia hukumu Jaji, hata kama una kesi ya namna gani, utapata upenyo tu! Wakati Rais anateua Majaji, kwa kweli ni hadhi maalum, wana ulinzi, wana usafiri na makazi ya kiongozi yasiyoingilika, pamoja na maslahi manono.
Bahati mbaya sijui kama Mh. Rais anajua huwa hawaandiki hukumu. Hukumu zinaandikwa na Mahakimu, yaani hakimu anaamua kesi yako, unajua ukienda kwa Jaji utakutana na akili kibwa iliyokomaa kwenye busara na sheria, lahaula, unakutana na Hakimu au anayeitwa msaidizi wa Jaji. Au Hakimu ambaye ni rafiki wa Jaji kwa hiyo anamtupia mafaili, Uwezo wao ukoje? Ni ile cream ya mahakimu au ni wale mfumo umewakataa?
Nani anashuhudia zile hukumu nzito nzito za majaji? Zipo, ila chache kulinganisha na juhudi za Rais kuteua majaji kwa kasi kubwa.
Tunataka Majaji waandike hukumu wenyewe, hawa wengine wanakosa tafakari pana ya sheria na jamii, na hawawajibiki wa yeyote, na pia si kumtendea haki mh. Rais kwa hadhi yake na imani aliyowapa.
Migogoro mingi tunayoona katika jamii ni matokeo ya Mahakama za Juu kutokutoa miongozo ya kisheria inayozungatia maslahi mapana ya jamii.
Jaji akikuta kosa dogo, halijalalamikiwa na yoyote ,halijaathiri haki ya msingi, kwa uvivu wa kusoma majalada, anaegemea hapohapo, anafuta kesi anaagiza ianze upya. Migogoro inakuwa inapanda na kushuka mahakamani.
Ina maana mahakama za enzi za akina Nyalali zilikwa haziyaoni makosa madogo madogo? Lakini zilikuwa zinazingatia jambo lililowaleta wadaawa mahakamani.
Sasa una kesi ya mabilioni au jinai nzito, hukumu inaandikwa na hakimu wa mahakama ya mwanzo au hakimu mkazi, unakutana naye disco huko unasema naye!