Jaji adai ubakaji ni kawaida kwa wanaume Waafrika

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,258
Image copyrightENOA
Image captionJansen amesema ujumbe wake umefasiriwa visivyo
Jaji mmoja mzungu nchini Afrika Kusini ameshutumiwa vikali baada ya kudaiwa kusema kwenye mitandao ya kijamii kwamba ubakaji ni kawaida kwa wanaume weusi.

Jaji Mabel Jansen alisema unajisi wa watoto na wasichana na pia ubakaji wa wanawake ni jambo la “kufurahiwa” la kupitisha wakati miongoni mwa Waafrika.

Kadhalika, amenukuliwa pia akisema hajawahi kukutana na msichana mweusi ambaye hajawahi kubakwa.

Kampeni imeanzishwa ya kutaka afutwe kazi.

Akijitetea, jaji huyo amesema amefasiriwa vibaya na kwamba matamshi hayo yametumiwa vibaya nje ya muktadha.

Jaji Jansen anadaiwa kutoa matamshi hayo kwenye mawasiliano na mwanaharakati Gillian Schutte kwenye Facebook mwaka jana lakini yamesambazwa sana wikendi.

"Katika utamaduni wao, mwanamke yuko hapo kuwaburudisha. Mwisho. Hutazamwa kama haki yao na mtu hatakiwi kuomba ruhusa kutoka kwa mwanamke,” jaji huyo amenukuliwa akisema.

Wakili mashuhuri Afrika Kusini Vuyani Ngalwana amesema matamshi hayo ya jaji huyo yanawaharibia sifa wanaume wote weusi na kuwaonesha kama wabakaji.

Amesema ni ya kushangaza sana, kwa mujibu wa gazeti la Business Day.
 
makubwa haya,huyu bibi atakua ,mbaguzi yani anamaanisha kua weusi ndio peke yao wabakaji weupe hawabaki? wakati na wao hawavumi lakini wamo na wana visa vya ajabu kupitiliza...
 
aisee, kwahiyo na yeye alishawahi kubakwa na mwanaume mweusi? amejuaje hao wanaobakwa hubakwa na waanaume weusi tu? huu ubaguzi wa hovyo sana kwa mtu anayeitwa jaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…