Izzo Bizness: Matukio ya Vifo na kutekwa na kupotea nchini, hali imekuwa ya kutisha zaidi

Waufukweni

JF-Expert Member
May 16, 2024
1,190
2,891
Rapa Izzo Bizness ameelezea hofu yake kuhusu matukio ya hivi karibuni ya vifo na kutekwa kwa watu, akisema hali imekuwa ya kutisha zaidi. Kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), Izzo ameonyesha wasiwasi kuhusu ongezeko la matukio ya kutoweka kwa watu nchini, huku akisema kuwa hali hiyo inasababisha hofu kubwa miongoni mwa wananchi.

Soma, Pia: TLS kuandaa kongamano la Kitaifa kuhusu matukio ya kutekwa na kupotea kwa raia nchini Tanzania

"Matukio ya vifo mara watu kutekwa na kupotea hali imekuwa ya kutisha zaidi," alisema Izzo. "Eeeh, MUNGU Baba Ibariki TANZANIA," aliongeza rapper huyo, akionyesha hisia za kuliombea taifa na kudhihirisha wasiwasi wake kuhusu usalama wa raia.
Screenshot 2024-12-06 112828.png
 
Back
Top Bottom