Kuandika mabango yenu kwa kiingereza mnatupoteza sie tusojua hiyo lugha, tunakuwa kama tupo Ulaya wakati ni nyumbani Tz, wito kwenu serikali kuu au halmashauri tuleteeni sheria inayopiga marufuku mabango kuandikwa kwa kizungu...Pia mabango yanayoelekeza huduma za jamii yawe na alama zinazoashiria huduma kama mlivyofanya rangi kwa daladala na taxi na magari ya shule.Tuithamini lugha yetu na tusiwabague wasiojua hicho kiingereza.Hapa ni nyumbani.