Itakuwaje watumishi wenye vyeti feki ikitokea wakapata tena ajira private?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,820
Wakati sasa tukiwa katika mjadala wa "VYETI feki "na wengine kufika hatua kuwasema vibaya waliofoji 'VYETI mitandaoni na wengine wakishangilia watu kuondolewa maofisini " kuna kitu ningependa kufahamu .

Hivi Leo hii ikitokea mtumishi aliyeondolewa serikalini kwa kashfa ya "VYETI FEKI" ivi itakuwaje ikitokea ameajiriwa tena katika mashirika ya private ambapo huko "UZOEFU WA NA UTENDAJI WA KAZI "

kwa mfano wakati yupo serikalini aliajiriwa kama mtu wa " IT au FINANCE "ikitokea ameajiriwa private kwa nafasi ile ile hapo sheria inasemaje """.

Je kama mwajiri wake amemwajiri kwa kuangalia kigezo cha UZOEFU na KAZI BILA KUANGALIA CHETI " YEYE AMEPENDEZEWA NA UFANISI WAKE WA KAZII ????

JE KATIKA HILO MNAZUNGUMZIAJE NA UPANDE WA PILI WAZIRI ANAWEZA KUFANYA UHAKIKI ???.
 
Hii mada ngumu sana kuijadili na kuizungumzia
Ila ukweli utabaki palepale kufoji cheti ni kosa la jinai ila ikitokea una cheti feki na umebahatika kuajiriwa private mashirika kama vile tigo,voda,airtel,e.t.c .
Uko wanangalia sana utendaji wa kazi sio cheti .
Kwaiyo kama ulitoka serikarini ukaenda private yote maisha.

Ila atayeumia roho ni yule alikucheka ukiwa katika wakati mgumu roho yake itamuuma sana akisikia ameajiriwa si unajua tena binadamu tusivyopenda maendeleo ya wenzetu
 
HII MADA INANIFANYA NIMKUMBUKE MWALIMU WANGU WA HESABU AIDEN PALE MCHIKICHINI .......

MSHIKAJI HAKUWAI KUSOMEA UALIMU ALISHIA FORM SIX TUU ILA NONDO ALIZOKUWA ANATOA SHULE KAMA LOYOLA,STMANTHONY WALIKUWA WANAMLILIA SANA
duu ivi aiden yupo aisee mshikaji alikuwaga nondo sana
 
Huko private hakuwahusu...wakae na ajira zao za serikali...
Ofisi ni zao..wao ndio wataamua wnataka nini..kwani serikali shida yao si kodi ilipwe...wawaaache.
Nimependa sana tofali ulivyoelezea kwa kweli ni kweli kabisa ni bora ukubali kuwachia ofisi uangalie maisha mengine.

Sasa hawa wanaoshangilia na kuwasema vibaya wenzao ivi unadhani wanajua wanachotenda
 

Kwani kuna sheria inayokataza kampuni ya private kuajiri kwa uzoefu?
 
Kwani kuna sheria inayokataza kampuni ya private kuajiri kwa uzoefu?
Mimi hata sifahamu ila nilichokuwa ninakilenga HAPA.

Ivi ukiwa private sector unaweza kuhakikiwa na serikari .

Na sheria inasema vipi ukitumia VYETI feki na ukifanya KAZI private
 
Mimi hata sifahamu ila nilichokuwa ninakilenga HAPA.

Ivi ukiwa private sector unaweza kuhakikiwa na serikari .

Na sheria inasema vipi ukitumia VYETI feki na ukifanya KAZI private
Inategemea na kazi.

Kwa mfano, kuna kazi zinazohakikiwa na bodi za kiserikali. Kazi kwa mfano kama za udaktari unatakiwa uwe na kiwango fulani cha elimu, sifikiri kama unaweza kuwa daktari wa upasuaji hospitali ya private bila kusomea udaktari. Kazi fulani za kihasibu zinaweza kutaka upite mitihani fulani ya kihasibu.

Kuna kazi nyingine za uongozi tu au mambo ya teknolojia watu wanaweza kuangalia kipaji na uzoefu zaidi kuliko vyeti.
 
Yaani tena private ndo zitawaajiri fasta, maana wanajua ni ngumu kwao kuhama. na wakiajiriwa watakuwa wanapiga kazi kinoma maana nyongeza pekee ya income yao itakuwa kutokana na performance na sio kumtisha muajiri kuacha kazi
 
Hapo alwatan nimekuelewa ulipozungumzia kipaji kwa mtu ambae yupo vizuli katika uongozi na technologia .

Kwaiyo hata akiajiriwa serikali haiwezi kuingiliaaa maamuzi ya private hata kama ana cheti feki.

Lakini fani yake sio ile kuhakikiwa kama daktari au nurse
 
Yaani tena private ndo zitawaajiri fasta, maana wanajua ni ngumu kwao kuhama. na wakiajiriwa watakuwa wanapiga kazi kinoma maana nyongeza pekee ya income yao itakuwa kutokana na performance na sio kumtisha muajiri kuacha kazi
Nimeipenda hii dah tena private anapata kazi dah acha TUU
 
Yaani tena private ndo zitawaajiri fasta, maana wanajua ni ngumu kwao kuhama. na wakiajiriwa watakuwa wanapiga kazi kinoma maana nyongeza pekee ya income yao itakuwa kutokana na performance na sio kumtisha muajiri kuacha kazi

yaan wew unajidanganya tu mabaraza ya taalum , kama pharmacy council, chama cha madaktari, maursy wakikupiga burn huewez kupractice sehem yoyote ile
 
wapo wengi tuu private wanamavyeti ya kutengeneza ila kazi wanafanya tuu japo kufoji ni kosa la jinai na ikibainika unafungwa so omba mungu akusaidiae.
 
Huko private hakuwahusu...wakae na ajira zao za serikali...
Ofisi ni zao..wao ndio wataamua wnataka nini..kwani serikali shida yao si kodi ilipwe...wawaaache.
....Hiki unachokisema leo kwenye malumbano ya hoja ITV Julius Mtatiro amelifafanua vizuri sana, kwamba kwa ujumla zoezi la vyeti feki ni jema na muhimu but approach is not correct. Amesema ilitakiwa zoezi hili lifanywe kote, including private sector, na kuwe na database ambayo hata ukiomba kazi private sekta na kupeleka vyeti waajiri wawe na uwezo wa ku access na ku verify vyeti vya muombaji. But ukisema zoezi ni kwa serikali tuu hao majority waliotumbuliwa watakimbilia private. Jana nimeona manesi wawili waliokuwa wanafanya kwenye hospitali ya wilaya na mwingine kituo cha afya wanafanya kazi kwenye hospitali ya private, tena kubwa tuu.
 
Yes thats right..serikali ilitakiwa iwe na system ya kuwa na data base ya kila msomi...ili kuepuka ujanja ujanja...na hili lingewazuia mpk wabunge na wakuu wa wilaya makanjanja kupata vyeo kwa kutumia kufoji vyeti...
Sasa since serikali yenyewe imeonyesha double standards nakuonyesha upendeleo wa wazi...wadeal na watu wao wa serikalin...walishachemka tangu mwanzo na system zao..ilitakiwa kila mtu mwenye cheti cha taaluma fulan ahakikiwe kabla ya kupewa ajira kokote kule...serikali imechemka tangu mwanzo..isilaumu watu...
Hata mimi kuna nurse namjua alitoka serikalini mwanzon tu mwa zoezi la uhakiki kaenda zake hospitali iliyoko baharini kule sew view ( ya wahindi) najua ushaisoma... and u know wht she was hard working...
Cheti cha form four ndio kilikua c chake lakini alienda kusomea taaluma ya unesi na akaajiliwa hospital tena ya taifa...
 
Hizo private sector (company)zinazoajiri mtu aliye kwenye list ya vyeti feki Hazijielewi
 
Wataamua wao huko huko, ila kuwadanganya mmmmmh!!

Muhimu wakumbuke serikalini mwisho tarehe15 Mei, kuachia ngazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…