Isingekuwa Lowassa CHADEMA wangepata kura ndogo sana Uchaguzi Mkuu 2015

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,698
8,558
Hakika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ulikuwa wa aina yake, haijawahi kutokea kwenye siasa za Tanzania haswa mara baada ya nguli wa siasa Lowassa kuhamia CHADEMA na kugombea Urais.

Nguvu ya Lowassa ilionekana waziwazi ndani ya chama chake alichokuwa, yaani CCM na hata nje ya Chama. Sio mchezo, Lowassa alikuwa na nguvu sana kiasi kwamba alipigiwa kura na vyama vyote, waliokuwa ndani ya CCM na CHADEM na hivyo kuvunja rekodi ya Mgombea wa upinzani kupata zaidi ya kura milioni 6 tangu vyama vya upinzani vianzishwe.

Pia CHADEMA hawatomsahau kigogo huyu maana wabunge wengi walipata ubunge kwa nguvu na ushawishi wa Lowassa halikadhalika madiwani.

Apumzike kwa amani mzee wetu Lowassa.
 
Binafsi naweza kutofautiana na maoni yako na wengi wanavyoona ila kikubwa ambacho naona uchaguzi wa mwaka 2015 ulikua ni uchaguzi wa kimageuzi tu wenyewe bila nguvu ya yeyote. Tena naweza sema pengine uwepo wa lowassa kwenye uchaguzi huo inawezekana umepunguza idadi ya hao wabunge au pengine Hata ndio ulikua wakati mzuri sana na upinzani kuchukua Dola mwaka huo.

Watu wengi walikua wamechoshwa na utawala wa CCM Kiasi kwamba walikua tayari kumchagua yeyote yule ambaye angekua mbadala wa CCM bahati nzuri au mbaya Chama tawala kilichanga karata zake vyema hatimaye kikashinda uchaguzi Tena na kuharibu system nzima ya Imani ya wananchi.

Siwezi beza nguvu ya Lowassa ila naona kungekua na mtu mwenye nguvu tofauti na yeye ( Asiye na makando kando ) nahisi tulikua tunaongea habari nyingene.
 
Kabla ya kuandika ungetafiti kwanza ujue huko nyuma Chadema ilikuwa na wabunge wangapi.
 
Naombeni ule wimbo wa msaga sumu aliomuimbia huyu marehemu

Ulikua wimbo wa taifa kipindi kile
 
Kabla ya kuandika ungetafiti kwanza ujue huko nyuma Chadema ilikuwa na wabunge wangapi.
Takwimu zipo wazi kabisa wala hakuna haja ya utafiti.
Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Chadema kama chama kikuu cha Upinzani kilipata viti vingi vya ubunge na udiwani zaidi kuliko chaguzi zingine.
hii ni kutokana na NGUVU ya mwamba huyu EL. r.i.p
 
Binafsi naweza kutofautiana na maoni yako na wengi wanavyoona ila kikubwa ambacho naona uchaguzi wa mwaka 2015 ulikua ni uchaguzi wa kimageuzi tu wenyewe bila nguvu ya yeyote. Tena naweza sema pengine uwepo wa lowassa kwenye uchaguzi huo inawezekana umepunguza idadi ya hao wabunge au pengine Hata ndio ulikua wakati mzuri sana na upinzani kuchukua Dola mwaka huo.

Watu wengi walikua wamechoshwa na utawala wa CCM Kiasi kwamba walikua tayari kumchagua yeyote yule ambaye angekua mbadala wa CCM bahati nzuri au mbaya Chama tawala kilichanga karata zake vyema hatimaye kikashinda uchaguzi Tena na kuharibu system nzima ya Imani ya wananchi.

Siwezi beza nguvu ya Lowassa ila naona kungekua na mtu mwenye nguvu tofauti na yeye ( Asiye na makando kando ) nahisi tulikua tunaongea habari nyingene.
Unaweza kuwa kweli lakini kumbuka kuwa CCM ilikuwa na hadi sasa inamtaji mkubwa wa wapiga kura kuliko chama kingine.
Huo mtaji ulimegwa na Mwamba huyo.
Kama isinge kuwa Lowasa Chadema wasinge pata hata kura milioni 3, huo ndio ukweli.
R.I.P EL
 
Back
Top Bottom