Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 401
- 1,023
Hali inakuwa si nzuri kwa vyama pinzani nchini kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa ambapo kila leo unasikia wanakutana na vibwanga. Leo ACT Wazalendo wanasema wagombea wao bila NIDA basi fomu awapati.
Mbona tuliambia kwamba uchaguzi huu utakuwa wa uhuru na haki! Lakini hali na kasoro kibao zimeanza kuonekana kuvunja haki na uhuru wa uchaguzi huu. Vipi sasa siku yenyewe ya uchaguzi hali itakuwaje?
============
Katika baadhi ya maeneo wagombea wetu (wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa) wametakiwa ili wapewe fomu ni lazima wapeleke vitambulisho vya uraia (National ID) ili kuthibitisha uraia wao vinginevyo hawapewi fomu, matukio kama haya yamejitokeza katika kata ya Kandawale, kijiji cha Mtumbei Mpopera kilichopo katika jimbo la Kilwa Kaskazini mkoani Lindi,
Zipo kasoro nyingi ambazo zimekuwa zikitokea katika hatua hii ya kuchukua na kurejesha fomu, ACT Wazalendo tunaamini kuwa matukio haya hayatokei kwa utashi wa wasimamizi wasaidizi wenyewe bali kwa maelekezo, tunazo taarifa kuwa baadhi ya Wakuu wa wilaya wameagizwa kuhakikisha kuwa ACT Wazalendo haashindi vijiji na mitaa katika uchaguzi huu na tumekuwa tunafuatailia kwa karibu juu mwenenndo wa uchaguzi, viashiria vinaonesha ukweli kuhusu taarifa hii na hasa katika mitaa ya jiji la Dar es salaam, kutokana na sababu 6hizo ACT Wazalendo tunataka hatua zifuatazo zichukuliwe, mosi Waziri ofisi ya Rais TAMISEMI awaondoe wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo yote yaliyoripotiwa kuwa na matatizo na wao hawajachukua hatua ya kumaliza tatizo hila" -Mchinjita
"Pili, katika siku hizi chache zilizobaki wagombea wa vyama vyote wachukue na kurudisha fomu bila ya kuwekewa vikwazo na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi maeneo ambayo wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi hawakutoa fomu au kuwa na mgombea wa mmoja kwa sababu ya wengine kuzuiwa makusudi kuchukua fomu uchaguzi wa maeneo hayo usifanyike mpaka watakapohakikisha waliojitokeza kugombea kwa mujibu wa sheria na kanuni wamepatiwa haki hiyo ya kugombea, mwisho ACT Wazalendo tunawaagiza wananchi pale ambapo wagombea wa vyama vingine wamezuiwa au kufanyiwa hila wasishiriki uchaguzi huo, wabebe jukumu la kuhakikisha wanatumia nguvu ya umma kuzuia uchaguzi katika maeneo hayo haufanyika mpaka kasoro hizo zirekebishwe" -Mchinjita
Soma Pia:
Isihaka Mchinjita ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Tanzania Bara amezungumza hayo alipokutana na wanahabari leo, Alhamisi Oktoba 31.2024

- CHADEMA Uyui Wanyimwa Fomu za Wagombea na Afisa Mtendaji
- ACT Wazalendo: Mawakala wa Vyama vya Siasa wanalazimishwa kwenda kuapa Halmashauri ambako ni mbali na maeneo wanayotoka