LGE2024 Iringa: UVCCM Glory Chambo awaangukia wananchi kwa magoti kuomba wawachague Wenyeviti wa CCM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,292
3,593
Wakuu,
Screenshot_20241125_205702_Instagram.jpg

Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM kutokea Mkoa wa Iringa Cde. Glory Chambo amewaangukia Wanamagulilwa kuomba wawachague Wenyeviti Wanaotokana na Chama cha Mapinduzi siku ya Uchaguzi Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba 2024.

Screenshot_20241125_205747_Instagram.jpg

Chambo amesema CCM ina haki ya kupewa muhula mwingine wa kuongoza Mitaa yote Tanzania kwani mambo iliyoyafanya yanaonekana kwa macho na si maneno.

“Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametekeleza kwa vitendo na si maneno.”
 
Wakuu,


Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM kutokea Mkoa wa Iringa Cde. Glory Chambo amewaangukia Wanamagulilwa kuomba wawachague Wenyeviti Wanaotokana na Chama cha Mapinduzi siku ya Uchaguzi Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba 2024...
Matapeli ya ccm yalisema chadema inacheleweaha maendeleo Leo yanakuja na hoja eti yachaguliwe ili yalete maendeleo wakati miaka mitano yalikuwa yenyewe shenzi kabisa.
 
Anawaangukia wajinga, Kilimanjaro ndio mkoa pekee sijawahi ona huu ujinga wa kupiga magoti na kulia, Hii inafanyika kwenye zone zilizo jaaa wajinga wa hili Taifa.

Na wajinga watamuelewa, watamuonea huruma, akitoka hapo anenda kulala hapo Iringa mjini hoteli ya nyota 4. wajinga wanaenda nyumani kulala njaa au kunywa uji au ugari mchicha.
 
Huu upumbavu wa kuwapigia magoti wapiga kura kwenye kampeni badala ya kueleza sera uliasisiwa na Magufuli pamoja na yule chawa wake. Hatimaye CCM wameurithi.
 
Back
Top Bottom