KERO Iringa mjini baadhi ya Adhana za misikiti zimezidi kelele, sauti iwe ya chini isiwe kero

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Matumizi ya Speaker ina mipaka yake. Ukizidisha sauti inakuwa sio adhana bali ni kero kwa wananchi, ambapo sio wote ni waislamu.

Dini yetu inasisitiza sana kuchunga haki za majirani na kwenye hili misikiti hawajapewa msamaha. Ifike mahali waendesha hizo misikiti wawe na aibu maana hakuna haja ya adhana ya msikiti mmoja inasikika zaidi ya kilometa 5 mtaa mwingine ambapo huko nako tayari wana msikiti wao kwani siku hizi kila mtaa/kata kuna msikiti wao.

Iringa ilivyo kwenye milima inafanya sauti itembee kwa umbali mkubwa yaani ECHO kwa kiingereza, hivo kuleta kero kwa wananchi.

Hatusemi waache kuadhini kwenye speaker, lakini sauti iwe ya chini isiwe kero.
 
Kikawaida adhana ni kuwaita waumini waende ibadani,ila mi napenda baada ya adhana mambo mengine yasikike ndani kwa ndani kama wanavyofanya Msikiti wa Taqwa Ilala Bungoni,wao wakiadhini basi,mambo mengine ya Ibada yanasikika ndani ya Msikiti tu.
 
Mambo mengine yaachwe kama yalivyo tuvumiliane tu,ni vitu vinapigiwa kelele kila siku miaka nenda miaka rudi hakuna muafaka.

Maana ukisema yule anapiga kelele utakuta hata wewe at some point kuna pahala unasababisha usumbufu kwa hao hao unaoona wanakupigia kelele.
 
Mambo mengine yaachwe kama yalivyo tuvumiliane tu,ni vitu vinapigiwa kelele kila siku miaka nenda miaka rudi hakuna muafaka.

Maana ukisema yule anapiga kelele utakuta hata wewe at some point kuna pahala unasababisha usumbufu kwa hao hao unaoona wanakupigia kelele.
Umeandika kitu kizuri sana Mtakatifu Anno II. Yatupasa tuvumiliane na tuchukuliane kwa kila jambo humu Duniani.
 
Jitihada zenu za kutaka nchi iwe ya Kikristo haitofanikiwa,kama alishindwa baba yenu mnayetaka aitwe Mtakatifu nyie takataka mliobaki hamtaweza.
Kuna haja gani ya kuita watu takataka? Tanzania haina dini moja, japo wakristo ndio idqdi kubwa zaidi, hapo analenga wapiga kelele wote kutia ndani walokole.
 
Kuna haja gani ya kuita watu takataka? Tanzania haina dini moja, japo wakristo ndio idqdi kubwa zaidi, hapo analenga wapiga kelele wote kutia ndani walokole.
Walokole wanapiga adhana! Acheni mambo yenu nchi hii kwa muda mrefu tumekuwa watu wa kustahimiliana maana kama kelele dini zote zimekuwa zinapiga kelele kwa namna tofauti mfano eneo nililokulia toka udogo wangu kuna kanisa Katoliki kengele zimekuwa zikipigwa kama ratiba ya chakula kwa siku kwa maana ya asubuhi, mchana na jioni tena kwa sauti ya juu lakini tumekuwa wavumilivu lakini pia kuna msikiti zinapigwa adhana kila muda wa swala na wenzetu wamekuwa wavumilivu pia kwa upande wao,halafu kuhusu hiyo idadi ya Wakristo kuwa ndiyo wengi siyo kweli maana hata waislamu kwa takwimu zao nao wanasema ndiyo wengi zaidi lakini hakuna takwimu sahihi zilizowahi kutolewa na chombo huru kilichoweza kusema waumini wa dini fulani ndiyo wengi zaidi.
 
Rwanda hiyo biashara ilifutwa na serikali. Unaangalia saa yako unakwenda msikitini finished!
 
Wacha watu wamuabudu Muumba wao,adhana yao ni dakika kadhaa tu ndugu wewe ikakukera Nini?Mbona makanisa yetu yanapiga mziki kutwa nzima wenzetu hawalalamiki.
 
Back
Top Bottom