Iran yakamata Meli 2 zenye bendera ya Tanzania zikidaiwa kusafirisha mafuta ya magendo

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
2,096
5,592
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limekamata meli mbili zilizokuwa na bendera ya Tanzania, zikidaiwa kuwa zilisafirisha mafuta ya dizeli kwa njia ya magendo katika Ghuba ya Uajemi,

Shirika la habari la Fars limeripoti kuwa meli hizo, zilizosafiri chini ya majina ya Sea Ranger na Salama, zilikuwa na lita milioni 1.5 za dizeli ya magendo na zilikamatwa na kupelekwa katika bandari ya Bushehr, kusini magharibi mwa Iran, kwa ajili ya hatua za kisheria.

Meli hizo pia ziliripotiwa kuwa na wafanyakazi 25 wa kigeni, ingawa taarifa kuhusu raia wao au hatma yao bado haijafafanuliwa.

Iran imekuwa ikishutumiwa mara kwa mara kwa kukamata meli katika Ghuba kwa madai ya usafirishaji haramu wa mafuta, hasa ikizingatiwa kuwa bei ya mafuta nchini humo ni ya chini sana duniani, jambo linalochochea biashara ya magendo ya mafuta kwenda nchi jirani.

Tukio hili linajiri miezi michache tu baada ya Iran kuwaachia huru wafanyakazi saba wa meli yenye bendera ya Ureno waliokuwa wakizuiliwa kwa madai ya uhusiano na Israel.

====================

Iran’s Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) has seized two foreign vessels carrying “smuggled” fuel in the Gulf, local media said on Tuesday.

The IRGC “seized two Tanzanian-flagged vessels carrying 1.5 million liters of smuggled diesel fuel,” said Iranian news agency Fars.

Iranian forces regularly target tankers they say are illegally transporting fuel in the Gulf.

“The vessels, Sea Ranger and Salama, had 25 foreign crew members,” said Fars, without elaborating on their fate.

It added that the vessels “were transferred to the port of Bushehr,” in Iran’s southwest, “for legal procedures.”

Iran, a major oil producer, has among the cheapest petrol prices in the world, which encourages fuel trafficking.

In May, Iran released seven crew members from a Portuguese-flagged container ship, seized on April 13, after accusing them of links to its arch-foe Israel.

Source: English Al Arabiya
 
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limekamata meli mbili zilizokuwa na bendera ya Tanzania, zikidaiwa kuwa zilisafirisha mafuta ya dizeli kwa njia ya magendo katika Ghuba ya Uajemi,
Nchi ya Zanzibar, ambao ndio wanayo mipango ya meli hizi wanayo bendera yao, kwa nini wasiitumie kwenye meli hizi?
 
Kwenye deals kama hizo, akina Abdul hawakosekani.

Ni bahati taarifa imetoka nje, ingekuwa ni hapa nje, hakuna chombo cha habari ambacho kingeandika, au wangebadilisha habari nzima kuonesha mama anavyolipigania taifa kuliletea mafuta ya bei nafuu.
 
Back
Top Bottom