Interplanetary Transport System[ITS]: Safari ya kwenda sayari ya Mars

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,370
3,956

Ule mpango wa binadamu wa kuweza kuishi nje ya sayari yake asili unaonekana uko mbioni kukamilika.

Kampuni binafsi ya Space X inayojihusisha na masuala ya anga(ambayo kwa sasa ina tender ya kupeleka mizigo kituo cha anga cha kimataifa) imepania kupeleka watu Mars ndani ya miaka 6 na baada ya miaka 50-100 tayari watakua wameanzisha mji(self sustainable city) katika sayari hiyo.

Safari ya kwenda Mars imepangwa igharimu kiasi cha $200,000 kwa mtu mmoja.Waliulizwa mbona na hela kidogo sana mtawezaje kufanya kitu kikubwa hivo?
Jibu lao liko katika mfumo wao wa roketi(ITS) ambayo inaweza kutumika zaidi ya mara moja tofauti na zile za NASA zinatumika mara moja tu kwa matumizi maalum.
ITS ina hatua mbili,hatua ya kwanza mashine nzima(Spaceship na Booster) inawashwa injini zikiwa 47 zinazotumia Methane zinapaa mpaka orbit ya dunia,Booster inajitenganisha na spaceship[inabaki inaelea angani] then inarudi duniani(Booster) inawekewa kichwa kingine(propellant) kilichojaa mafuta inarudi mpak orbit inajaza tank ya spaceship iliyokua inaelea orbit. Hatua ya pili inaanza kwa spaceship iliyojazwa mafuta kuanza safari yake ya miezi 6 kuelekea sayari ya Mars.

Safari ya Mars itakua inafanyika kila baada ya miezi 26 ili kuivizia sayari ya mars ikiwa karibu na dunia katika harakati zao za kuzunguka jua

Kwa nini iwe Mars na sio kwenda kua wakoloni wa mwezi?

Mars ina rasilimali nyingi ambazo pia zipo duniani.
Ina gravity ambayo ni theluthi ya gravity ya dunia
Siku yake ina masaa 24 na dakika 40
Ina atmosphere
 
Duh..safari ya mwanza dsm..masaa 14 hivi ila inachosha balaa..sasa hiyo ya miezi sita tena kwa roketi si majanga mtupu...
 
ndo inakuaje hii
Space X wanasema sababu kwa sasa haiwezekani kwenda mars,basi cha kwanza kufanyika kiwe kwenda kwanza ndio milango mingine itafunguliwa;

Mambo kama huo mji utajengwaje,watatumia nishati gani,watatengeneza vipi chakula ,watakua na uraia gani vitajulikana baadae.
 
sasa haiwezekani kwenda alafu inabidi waende, wanaendajhe?
 
sasa haiwezekani kwenda alafu inabidi waende, wanaendajhe?
Hujaelewa kidogo
Kwani ushawahi kusikia mtu kafika mars mpaka sasa?Wamejioa timeframe ya miaka 6 wawe wanepeleka watu huko.sasa kama hakuna mtu kaenda huko unaongeleaje uraia kabla hata hunafika??
 
Kuna kitu kinakwamisha apo pia, utengenezwaje wa oxygen kwa ajili ya kupumulia, kuna research na design mbali mbali ambazo hazijapitishwa rasmi ili kutumika. na jamaa wako sereous kweli
 
Duh..safari ya mwanza dsm..masaa 14 hivi ila inachosha balaa..sasa hiyo ya miezi sita tena kwa roketi si majanga mtupu...
Kweli wapo watu wanaongelea suala la hayo mambo ya psychology kama haya..Binadamu hajazoe kuishi katika sehemu ndogo kwa mda mrefu bila ya kua na mahali pengine pa kwenda.ingawa spaceship iko comfortable ni kama nyumba lakini bado..

Hii ni safari kwa ajili ya humanity,huwezi jua vitagunduliwa vitu gani kama binadamu akiwa multiplanetary species.

Whoever discovered Americas angekua anaogopa kupanda meli kwa mda mrefu wasingegundua kua kuna dunia nyingine
 
Hujaelewa kidogo
Kwani ushawahi kusikia mtu kafika mars mpaka sasa?Wamejioa timeframe ya miaka 6 wawe wanepeleka watu huko.sasa kama hakuna mtu kaenda huko unaongeleaje uraia kabla hata hunafika??
kabla ya kuanzisha kitu lazima utakuwa na full details ili isije kuleta shida na mataifa mengine kumbuka kule pia wanaenda kuanzisha miji lazima wataweka uongozi, ni lazima wamepanga utaratibu utakuaje, pia kunauwezekano wa kwenda na kutorudi tena. so lazima kule wameandaa utaratibu wa kuingia na kutambulika kama nchi zingine zifanyavyo
 
Kuna kitu kinakwamisha apo pia, utengenezwaje wa oxygen kwa ajili ya kupumulia, kuna research na design mbali mbali ambazo hazijapitishwa rasmi ili kutumika. na jamaa wako sereous kweli
Oxygen inaweza kutenganishwa kutoka Carbon dioxide ambayo inapatikana kwa wingi katika atmosphere ya Mars.
 
Ndani ya miaka 50-100 mambo yote yatakua yamekaa sawa.Hii ni kampuni binafsi inataka kupeleka watu huko.Kama vipi anzisha kampuni yako itakayo shughulika na mambo unayoyasema.
 
Ndani ya miaka 50-100 mambo yote yatakua yamekaa sawa.Hii ni kampuni binafsi inataka kupeleka watu huko.Kama vipi anzisha kampuni yako itakayo shughulika na mambo unayoyasema.
Mi kampuni yangu itapeka makoti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…