Internet service provider

edwin89

Member
Apr 12, 2016
92
99
Habari wana jukwaa. Natangaza huduma ya mtandao majumbani na maofisini kwa vifurushi nafuu kabisa. Huduma hii itaanza kuanzia mwezi wa 10 mwishoni mara tu baaada ya kukamilisha vibali vya serikali.
Walengwa ni kama ifuatavyo-Majumbani, Maofisini, Stationery, Pharmacy.

Maeneo ambayo tayari miundo mbinu imefika.: Tegeta, Mbweni, Makumbusho, Kinondoni, Kijitonyama, Mwananyamala, Mikocheni, Kawe, Sinza, Magomeni, Msasani, Masaki, Morroco, Mwenge, Makongo juu...

Tafadhari karibu kwa maulizo na maombi na utaje sehemu uliyopo. Kauli mbiu yetu mteja ni dhahabu kwetu. Ahsante.
 
Hivi kwanini kila mtu anayeanza ku supply internet coverage ya kwanza lazima ipelekwe maeneo hayo?

Kwa maoni yangu naona hayo maeneo tayari yamejitosheleza kwenye huduma za internet kutokana na makampuni mengi kuwekeza huko.

Makampuni yamekuwa mengi kuliko uhitaji wa watu.

Wakati maeneo kama Vingunguti, Buza, Kiwalani, Gongolamboto, Kigamboni nk yana watu wengi wenye uhitaji wa internet lakini hakuna hata kampuni lililo invest huko kutoa huduma ya internet.

Hayo maeneo mliiyofika tayari kuna Fiber kama zote, wengine na Head Quarter zao zipo hapo hapo.
 
Yaani mfano Zuku wangekuwa wamefika Kibamba, Mpiji Magohe, Mbezi Msakuzi nk wangezoa sana wateja. Sawa ni nje ya mji ila siku hizi wakazi karibu wote wana smartphones, na smartphone bila internet - hakuna kitu. Makampuni ya simu bei zao ni katili ila wananchi wanakomaa nazo. Wawekezaji fungukeni, wateja wapo.
 
Mafanikio Prepress Network. Tutafika kaka tunatakiwa kuwa na maombi yasiyopungua 10 tunafunga Mnara kwenye ghorofa refu ili iweze kuwafikia. Tunasubiria leseni ya TCRA itoke tuingie mtaani kuwatafuta wateja
 
Ofisi yetu kuu ipo Mwananyamala koma koma jengo la biashara complex pale karibu.
 
Punguzeni bei kidogo, na sisi wenye kipato cha chini tuweze kumudu
 
Tupo mpaka Buza mkuu,
Ukijibu hivi ni ngumu kuona.

Jitahidi uwe una quote post husika ili tupate notification.

Buza mmefika lakini hapo juu haujaandika, ni kama Dar Es Salaam ina wahusu watu wa maeneo hayo tu.

Package zenu zipoje?
 
Back
Top Bottom