Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 14,680
- 54,907
Mama Salma alipendekeza kuwa wanandoa wa viongozi nao walipwe kama vile ambavyo "wapenzi" wao wanalipwa. Rais Samia Suluhu Hassan akaona hilo ni wazo zuri na akaamua kulifanyia kazi kwa kuunda muswada na kuupeleka bungeni. Sasa hivi, imekuwa sheria. Kwa hiyo, katika nchi hii, tuna wake wa viongozi wanalipwa simply because ni wake wa viongozi.
Siyo kwamba zamani haukuwepo utaratibu wa kuwatunza wajane wa viongozi, la hasha, ulikuwepo. Lakini Mama Salma akaona kwamba yeye anavyomhudumia Mzee Kikwete basi anatufanyia sisi Watanzania favor na kwa hiyo tunastahili kumlipa mpaka siku yake ya mwisho duniani!
Wakati mzee Kikwete anamchumbia, hakutushirikisha, wakati anamtolea mahari hakutushirikisha. Lakini leo Mama Salma anaona kuwa sisi Watanzania tuna deni kwake, kwamba ni lazima tumlipe simply kwa sababu yeye ni mke wa JK, mzee maarufu, muungwana!
Wakati anapendekeza hayo, huyo mama ni mbunge, mumewe ana mijihela kutokana na marupurupu kibao ya urais, mtoto wake ni mbunge. Sijui alikosa nini hadi kutaka apewe kingine juu ya kingi alicho nacho!
Leo nchi inahangaika kukamua wafanyabiashara, kodi zimekuwa mzigo, tozo zimekuwa nyingi. Miongoni mwa hizi pesa zinazotafutwa ni ili ipatikane pesa ya kuwalipa akina mama Salma kwa kuwa tu ni wake wa viongozi!
Najiuliza, mambo haya ya ajabuajabu hivi yagetokea Kenya, Wakenya wangeyaruhusu kweli? Kwamba mke wa rais mstaafu alipwe simply kwa sababu alikuwa mke wa rais? Hivi hawa watu wanatuchukuliaje sisi?
Watawala wa CCM wanadhani kiburi chao cha kutoheshimu hisia na mawazo ya Watanzania hakiwezi kuwa challenged. Lakini wasichokijua ni kuwa Watanzania WANADOCUMENT dharau moja baada ya nyingine, ujinga mmoja baada ya mwingine. Siku WAKIKINUKISHA, hayahaya mambo wanayodhani wamesahau ndiyo watakayowaambia kuwa wamechoshwa nayo. Hayahaya ambayo watawala wanadhani Watanzania wameyasahau na kwa hiyo kudhani kuwa wanaweza ku "go away with," ndiyo yatakayosomwa mbele ya vyombo vya habari siku hiyo kuwa ni sababu ya maamuzi yaliyofikiwa!
CCM wamekuwa too arrogant now. Watawala hawaogopi wala kujali wananchi kabisa! Kikombe cha gadhabu za Mtanzania kinaendelea kujaa polepole. Ole wao siku hiyo ya hasira kali itakapofika. Tanzania si kisiwa!