Last KING Ontuzu
JF-Expert Member
- Jul 22, 2016
- 628
- 894
Ingekuwa huko Galilaya ya kale uwezekano wa Trump kushinda uchaguzi Marekani ungekuwa ndoto ya mchana, angekumbana na nguvu ya dola na kila aina ya mfinyo kuhakikisha mgombea wa chama tawala bi Kamala Harris anashinda.
Kwanza siku ya uchaguzi jana na leo mitandao ingekuwa imezimwa huku vyombo vya habari vikipigwa marufuku kuripoti matokeo tofauti na yale yanayotangazwa na tume iliyo chini ya serikali pekee, tume inayofanya kazi kwa maelekezo ya serikali yenye mgombea pia
Huenda wagombea wengi wa upinzani wangekuwa vizuizini kwa kisingizio cha viashiria vya uvunjifu wa amani na intelijensia, matukio ya mabox ya kura feki na baadhi ya wahuni kutokomea na masanduku ya kura yangeripotiwa
Hiyo ndio tofauti ya demokrasia iliyostaarabika na demokrasia za kihuni ambazo wahuni bado wana nafasi ya kufanya figisu za kila aina kujitangaza washindi.
Hiyo ndio Marekani inayoishi katika misingi ya demokrasia na maamuzi ya wananchi, sio maamuzi ya wahuni wachache wenye nguvu wanaopanga matokeo watakayo
Marekani uchaguzi ni amani sio vita, mitaani hapajaonekana magari ya washawasha na wanajeshi wakijiandaa kukabili raia
Uchaguzi wao upo HURU, HAKI NA WAZI
Kuna tofauti kubwa mno bado kati ya NURU na GIZA