jikuTech
Senior Member
- Apr 9, 2023
- 138
- 194
LUGHA ZA PROGRAMU
Programu hizi zimeandikwa kwa kutumia lugha za programu. Hapa kuna baadhi ya lugha za programu.- Python
- Java
- C++
- JavaScript
- Ruby
- C# n.k
Lugha za programu ni kama lugha za kibinadamu lakini zimeundwa kwa ajili ya mawasiliano na kompyuta. Ni seti ya sheria na syntax ambazo tunatumia kuandika maelezo ambayo kompyuta inaweza kuelewa na kutekeleza.
Kwa nini tunahitaji lugha za programu ?
Kompyuta ni mashine za kihesabu ambazo zinaweza kufanya kazi kwa kasi kubwa sana, lakini hazina uwezo wa kufikiri au kuelewa lugha ya kibinadmu kama Kiswahili au kiingereza . Lugha za programu hutasaidia kuwasiliana na kompyuta kwa njia ambayo zinaweza kuelewa na kutekeleza maagizo yetu.Python: ni lugha rahisi kujifunza inatumika sana kwenye ujasusi (hacking ) , sayansi ya data (data science) na utengenezaji wa tovuti ( web Development)
Java: Hii ni lugha yenye nguvu sana na inatumika sana katika utengenezaji wa programu za Android na Programu za biashara kubwa.
Pamoja kompyuta inaelewa lugha za programu nazo lugha hizi zina eleweka na kompyuta baada ya kutafsriwa , mtafsri wa lugha za programu ili ziweze kueleweka na kompyuta anaitwa Compiler ni software ya ndani maalumu kutafsri au kubadilisha lugha za programu ili kueleweka na kompyuta. View 11
Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja