Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 30,680
- 34,079
Viongozi, mgombea au mtendaji wa Chama cha Siasa, mwanachama na mfuasi wa Chama cha siasa kulingana na Kanuni za maadili ya uchaguzi Mkuu zilizochapishwa hii leo kwenye gazeti la Serikali tayari kutumika, ni marufuku kuhamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika uchaguzi mmoja, kununua kadi ya mpigakura. Kukusanya kadi za wapigakura ama kuharibu kura.
Watu hao pia hawaruhusiwi kutoa hongo, zawadi, kununua kura, shukrani au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpigakura au mtendaji wa uchaguzi, kuhamasisha au kuzuia wapigakura wasijitokeze kupiga kura siku ya kupigakura ama kuvamia au kukaa kwa nguvu ndani ya kituo cha kupigia kura, kuhesabia au kujumlishia kura.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha Mtu yeyote hatoruhusiwa kutumia simu ya kiganjani au kifaa kingine cha mawasiliano ndani ya kituo cha kupigia kura, kuhesabia au kujumlishia kura isipokuwa kwa msimamizi wa uchaguzi, msimamizi msaidizi wa uchaguzi, msimamizi wa kituo, wasaidizi wake na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao wataruhusiwa kutumia simu zao au kifaa kingine cha mawasiliano pale itakapobidi kwa shughuli za uchaguzi tu.
"Simu na vifaa hivyo kwa wakati wote viwe vimeondolewa mlio na viwe kwenye mtetemo" imesema Kanuni ya maadili ya uchaguzi Mkuu 2025.