Inawezekana kweli laana ya mwanake uliemuacha kwa makusudi ikanipata?

Maleven

JF-Expert Member
Sep 8, 2019
666
3,204
Nilikua na mahusiano na binti, tulikua wadogo yeye O level mimi advance, alinipenda kwa dhati ila mimi nikiri sikua najua maana ya upendo na maumivu yake, nilipomaliza advance nilimuacha tu bila kosa.

Alilia wiki nzima lakini nilichukulia kawaida sana kwanza niliamini ni kama maigizo, aliendelea kuniomba nisimuache kwa miezi kadhaa mpaka mwaka wa kwanza chuo hakukata tamaa, ila kauli yake ya mwisho ni kua “ na wewe utapata atakae kutesa kama ulivyonifanyia”

Tangu hapo asilimia kubwa mimi ndo mimekua nikipenda, yani ndio naonekana mwenye uhitaji sana. Hata kwa wanawake ambao nimewazidi elimu kipato n.k bado ni kizungu mkuti, kwa sasa hata unyumba napewe kwa mbinde.

Yule msichana ameshaolewa na sijui anaishi wapi, ila natamani ningemuba msamaha, mana nilipigwa tukio niliumia mpaka niliwaza kufa, sasa naelewa maumivu alioyapata yule bint.

Kokote uliko SM wa Kilakala nisamehe, Sincerely MR Mzmb
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom