Binafsi siamini kuwa serikali hii ya sasa, kama ilivyokuwa kwa serikali zilizopita, hawaelewi kuwa ukipinguza kodi ya kuingiza magari nchini, watu wengi zaidi wataagiza magari na hivyo kuiongezea zaidi serikali mapato, bali naamini wanahofia miundombinu ya jjji kuzidiwa na wingi wa magari ila hii imekuwa ni siri yao.
Hali hii ni kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya magari hubaki jijini Dar-es-Salaam (Jiji la Ilala) na asilimia ndogo tu ndi huenda mikoani.
Hivyo, ukishusha kodi, kuna uwezekano baada ya muda uingizaji wa magari kuongezeka kwa kasi na kufanya baadhi ya barabara za jiji kuwa na foleni kubwa zaidi na hiki ndio serikali huenda wanakihofia kwani mpaka sasa tatizo la foleni katika huu mji teyari ni tatizo na kero kubwa kwa wakati wa huu mji.
Kama kodi ya kuingiza magari nchini ni karibu bei ya kununulia gari huko nje, ni wazi ukipinguza kodi ya kuingiz magari kwa asilimia kubwa mfano kwa asilimia 25 a tu, watu wengi zaidi watamudu kuingiza magari na kuongeza mapato ya serikali lakini kuna hatari ya miundombinu kushindwa kuhimili ongezeko hilo hasa nyakati za asubuhi na jioni kwani private car zinaweza kuongezeka kwa kiwango kikubwa.
Wenye fedha zao watauza magari yao kwa wingi humu nchini ili waagize mengine ya kisasa na bora zaidi (new model, n.k), na hivyo kuongeza magari used ya kibongo na wakati huo huo kupelekea ongezeko la magari used kutoka nje.
Pia, tutarajie ongezeko la magari ya mikopo kutoka kwa wafanyakazi wa serikali na wa sekta binafsi na kwa maana hiyo kutakuwa na ongezeko kubwa la magari hasa Dar-es-Salaam na ongezeko kubwa la mapato ya serikali kupitia kodi ya uingizaji wa magari lakini barabara za jiji zikizidiwa.
Kwa Dar-es-Salaam magari mengi yanaonekaba kuwa na plate number mpya na hiki kinaweza kuwa ni kiashira tosha kuwa sehemu kubwa ya magari (hasa ya kutembelea) hubaki Dar-es-Salaam na asilimia ndogo ndio huenda mikoani na hivyo kuchangia kukua kwa tatizo la foleni jijini Dar-es-Salaam (Ilala)
Hivyo, kwa mtazamo wangu, ugumu wa serikali kupunguza kodi ya kuingiza magari inawezekana inatokana zaidi na hofu ya kuongeza kwa foleni za magari jijini Dar-es-Salaam pamoja na siku moja tukafikia hatua ya magari kushindwa kutembea kabisa hasa nyakati za asubuhi na jioni.
Kwa maneno mengine,serikali kutoza Kodi kubwa za uingizaji wa magari lengo sio serikali kukusanya mapato mengi, bali yawezekana lengo hasa ni kudhibiti uingizaji wa magari nchini wakilenga jiji la Dar-es-Salaam.
Kama hii ndio hasa concern yao, basi wapunguze kodi ya magari yasiyo ya kutembelea (malori,mabasi,n.k) na ikiwezekana kwa magar yanayoingizwa nchini na kisha kupelekwa mikoani ingawa hii inaweza kuwa ni uchochoro wa watu kukwepa kodi kwa kuingiza magari wakida yanakwenda mikoani halafu baadae wakayarudisha jijini unless uwekwe utaratibu maalumu wa kudhibiti unadanganyifu huo unaoweza kujitokeza.
Ni mtazamo wangu pia hata uamuzi wa serikali ya Magufuli kuharakisha kuhamia Dodoma, umesukumwa pia na dhamira ya kupunguza foleni katika jiji la Dar-es-Salaam ingawa serikali haiwezi kukiri hadharani.
No wonder pia serikali imekuwa tayari kutumia mabilioni kujenga daraja la kupita juu ya bahari lengo likiwa ni lile lile la kupunguza foleni na kuwaondolea adha ya kukaa foleni wakubwa wanaoingia na kutoka katikati ya jiji.
Ukisikia siri za serikali au za usalama wa nchi, basi inaweza kuhusu mambo kama haya, mambo ambayo watu wengi wala hawawezi kuyafikiria wala kuyawaza, ila wao kama serikali kwa kutumia data walizonazo, wanakuwa wameshaona hatari ya nini kinaweza kutokea.
Wengi hamtanielewa ila huu unaweza kuwa ndio ukweli wenyewe kwa wanaotazama mambo kwa umbali.